• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Jinsi ya Kupata Kibali Cha Ujenzi

KIBALI CHA UJENZI

Kibali cha ujenzi ni Moja ya kanuni muhimu sana ya upangaji wa miji nchini Tanzania. Kila anae hitaji kujenga anapaswa kufuata kanuni za ujenzi katika kibali cha ujenzi atakachopewa, mara nyingi kwa mujibu wa sheria kibali cha ujenzi hutolewa na mamlaka za serikali ambazo ni halmashauri kupitia idara ya mipango miji na mazingira.

UTARATIBU WA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI

Kibali cha Ujenzi ni kibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenzi holela mijini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wa jengo.

UMUHIMU WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI

•Kutimiza matakwa ya kanuni za ujenzi mijini

•Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yalivyoelekezwa katika mipango miji ya sehemu husika

•Kudhibiti ujenzi holela

TARATIBU & KANUNI ZA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI

Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. Report submitted for Approval (RPA)”. Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao;

•Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector)

•Afisa Ardhi (Land Officer)

•Mpima (Land Surveyor)

•Afisa Mipango Miji (Town Planning Officer)

•Afisa Afya (Health and Sanitation Officer)

Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “Architectural & Structural Drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyoonyeshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki kama ifuatavyo.

Mkaguzi wa Majengo (Building Inspector) – kuona kama michoro inakidhi haja ya kiufundi na specifications.

Afisa Ardhi (Land Officer) – kuona kama umiliki wa eneo linaloendeleza ni halali, kukagua hati miliki, nk.

Mpima wa Jiji (Land Surveyor) – kutambua mipaka halali

Afisa Mipango Miji wa Jiji (Town Planning Officer) – Kuona kama ujenzi unaoombewa ni sahihi kwa mujibu wa michoro ya mipango miji.
v.Afisa Afya (Health and Sanitation Officer) – kuona kama usafi kwa ujumla na maji taka yatatunzwa vyema

Kama michoro na nyaraka za umiliki zimekidhi vigezo zitawasilishwa kwenye kamati ya mipango miji na utoaji vibali vya ujenzi.

Baada ya michoro na nyaraka kupita katika kamati ya mipango miji na utoaji vibali itapigiwa makadirio na mwombaji atapaswa kulipia gharama husika kwenye akaunti ya Halmashauri atakayopewa.

Mwombaji kuandaliwa kibali cha ujenzi kinachosainiwa na mhandisi wa ujenzi na afisa mipango miji

MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI

•Endapo mwombaji atakamilisha hatua zote muhimu kwa wakati atapata kibali cha ujenzi ndani ya majuma mawili (2) hadi manne (4)

•Hii ni pamoja na uwasilishaji wa ramani zilizoidhinishwa na wataalamu husika na hati za umiliki zilizo sahihi.

WAJIBU WA MWANANCHI

•Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga au kukarabati nyumba yake iliyo ndani ya mji/jiji kwa kibali kutoka Halmashaur

TAHADHARI

•Endapo mwananchi yeyote atajenga au kukarabati nyumba bila kibali cha ujenzi toka Halmashauri, atapewa ilani ya kusimamisha ujenzi au ukarabati na kushauriwa kufuata taratibu za kuomba kibali cha ujenzi ndani ya siku saba (7)

•Kama mwombaji atakaidi ilani ya kusimamisha, jiji au mji litampa ilani ya kubomoa jengo lake mwenyewe na akishindwa jiji litabomoa jengo husika na kudai mmiliki gharama za utekelezaji wa ubomo .

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa