• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Ustawi wa Jamii
    • Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Upimaji wa Ardhi

HATUA ZA UPIMAJI ARDHI


ARDHI yoyote ile ili kutumika kwa matumizi endelevu Ni Bora kuipangilia matumizi na namna ya kuitumia, ukifanya hivyo Ardhi yako itakuwa inatumika kwa utaratibu maalum tofauti na mazoea.

Watu wengi wamezoea kutumia ardhi kimazoea kwa kuwa tangu amezaliwa ana iona ardhi na anaitumia bila kupima Wala kupangwa na mambo yanaenda vizuri tu, lakini nikwambie kitu kimoja tu rafiki yangu, ardhi isiyopimwa haimilikiwi na mtu na ipo chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maana yake siku akipata matumizi ya hiyo ardhi unayoitumia atakuja kuipima na kuanza kutekeleza matumizi yake ambayo Mara nyingi huwa Ni uwekezaji, biashara au kujenga huduma za jamii.

Hivyo kumbe tunapaswa kuacha kuitumia ardhi kimazoea na badala yake tuitumie kisheria na kufuata taratibu zote zilizowekwa na sheria zetu.

Miongoni mwa hatua za upimaji ardhi, moja kubwa ni utambuzi wa eneo kijiografia na uandaaji wa Ramani (mchoro wa mipango miji).


Nini maana ya utambuzi wa eneo kijiografia?

Maana ya utambuzi wa eneo Ni kitendo Cha kuainisha kipande Cha ardhi Katika uwanda wa dunia, pia Ni kitendo Cha kusajiri kipande hicho Cha ardhi Katika sattelite za dunia ili kuepuka miingiliano ya kimaeneo duniani.

Kitendo hiki hufanyika kwa kutumia vifaa maalumu na vya kisasa vyenye uwezo wa kuchukua alama za kijiografia Katika eneo husika na kulihusinisha na alama za kijiografia kidunia, vifaa hivyo vinajulikana kwa majina ya GPS au RTK na wakati mwingine ndege zisizo kuwa na rubani “drones” hutumika kupiga picha ya anga eneo Hilo.

Hivyo hatua hii ni muhimu Sana Katika upimaji wa eneo lako na hatua hii hufanywa pia kwa makusudi ya kupata taarifa muhimu za kuandalia mchoro/Ramani ya mipango miji.


Nani anahusika na hatua hii?

Mhusika ambaye Ni mtaalamu wa uchukuaji taarifa hizo ambaye pia ndie anaye husika na uandaaji wa Ramani za mipango miji Ni afisa mipango miji yaani “TPO”. Mara nyingi kumekuwa na miingiliano ya kimajukumu Kati ya mpima na Afisa mipango miji. Hivyo nakusihi kuwa zoezi Hili hufanywa na Afisa mipango miji Wala sio mpima Kama wengi wanavyofanya.

Mara baada ya utambuzi wa eneo lako kijiografia, kinachofata Ni mtaalamu wa mipango miji ataanda ramani/ mchoro kupitia taarifa alizozipata site.


Nini maana ya mchoro/ Ramani ya mipango miji.?

Hii Ni ramani maalum inayoonesha matumizi ya eneo lako na matumizi hayo yanaweza kuwa makazi, biashara,kiwanda,taasisi, maziko, kilimo au burudani.

Mtaalam anayeandaa ramani hii Ni Afisa Mipango miji Na baada ya kuandaa atapeleka Katika ngazi zote za kiutawala kwenda kusajiri na kuidhinisha matumizi hayo.

Baada ya kufanya hatua hizo za utambuzi na uandaaji Ramani ya matumizi ya ardhi yako, sasa ndipo ramani hiyo imfikie mpima na ataitumia Kama muongozo wa kupima ardhi yako.


Ni Nini maana ya kupima ardhi?

Maana ya kupima ardhi Ni kitendo Cha uwekaji vipimo uwandani, kwa maana ya urefu na upana wa eneo lako ma baada ya kupima mtaalamu mhusika ambaye Ni mpima ata hakikisha vipimo hivyo vinapata usajiri na kuidhinisha na idara ya upimaji ardhi iliyopo Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Akishapata usajiri atapatiwa namba ya kiwanja chako ikiwa Ni pamoja namba za vigingi (beacon) na atakuja kuvizika Katika eneo lako Kama kielelezo Cha kupimwa hiyo ardhi na namba za vigingi (mawe/beacon) hazijirudii dunia nzima, hivyo Ni tofauti na za mtu mwingine sehemu yoyote ile duniani.


Namna kazi inavyofanyika

Kazi hii ya kutekeleza hatua za upimaji ardhi zinafanyika kwa ushirikiano mkubwa Kati ya Afisa mipango miji, mpima na mamlaka za kiutawala. Hata hivyo Mara nyingi ukiwa na eneo lako una mkabidhi kazi eidha Afisa mipango miji au mpima na yeye ndiye atakaye hakikisha Eneo lako linapata vitu vyote muhimu kwa mujibu wa sheria lakini Kama huna kiasi Cha fedha Cha kukidhi gharama za kazi hizo basi anza na utambuzi wa eneo halafu andaa mchoro/ Ramani ya matumizi ya ardhi yako na baadae malizia kupima.


Nini kina fuata baada ya kupima?

Kwanza kabisa fahamu kuwa kielelezo Cha kuwa eneo lako limepimwa na kupewa namba ya kiwanja chako pamoja na namba za mawe yako. Baada ya hapo kufuatia namba ulizopewa Anza kutafuta hati ya kumiliki eneo lako.

Anza Sasa kutafuta uwezekano wa kupima eneo lako, ona kupima kunavyo kuwa muhimu Katika misingi ya kusimamia sheria bila shuruti.

Ona namna unavyoweza kuwa mkimbizi Katika ardhi yako usipo Pima, ona namna unavyo weza kupoteza Haki zako na za watoto wako usipo Pima ardhi yako, ona namna unavyopoteza fursa za kumiliki eneo lako usipo Pima eneo lako.

Ni matumaini yangu utahamasika na kuelimika juu ya upimaji wa ardhi.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya Katibu Muhtasi na Madereva Halmashauri ya Mji Kondoa February 24, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha nne Shule za Halmashauri ya Mji Kondoa January 29, 2023
  • Waliochaguliwa na shule walizopangiwa kidato cha kwanza 2023 Kondoa Mji December 14, 2022
  • Tangazo la kazi December 07, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mhe. Rais, Ditopile watoa milioni 15 kwa Wanawake wa Vikoba Kondoa

    March 13, 2023
  • "Shirikianeni watoro warudi shuleni"- Mkurugenzi Sweya

    March 09, 2023
  • RC Senyamule aongoza Wanawake wa Dodoma kuadhimisha siku yao Duniani

    March 08, 2023
  • Madaktari bingwa wawashauri wananchi kuchunguza afya mapema

    March 05, 2023
  • Tazama Vyote

Video

Fursa za uwekezaji Kondoa Mji
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa