• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Aliyevamia eneo la stendi Bicha apewa siku saba kuvunja nyumba

Tarehe iliyowekwa: September 2nd, 2022

Mwananchi aliyejulikana kwa jina la Mohamed Fonga aliyevamia na kujenga eneo la mradi wa viwanja vya stendi ya Bicha amepewa siku saba kuvunja nyumba aliyojenga kwa kuwa alishapewa fidia ya eneo hilo shilingi milioni 40 hapo awali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Mamba Sweya wakati  kamati ya fedha na Utawala kwa ajili ya kukagua mali za Halmashauri ilipofika kukagua eneo la mradi wa stendi ya Bicha hivi karibuni.

“Cha pili tunamtaka arudishe mabati aliyoiba katika choo cha stendi, matofali na fremu tatu za milango zilizokuwepo katika eneo la mradi na sitaki kumuona ofisini kwangu kuhusu suala la hapa ila akija kama mwananchi mwingine nitamuhudumia kwanza tumefahamiana kwa kuwa migogoro wakati mwingine inaleta hali ya kufahamiana,”amesema Mkurugenzi Sweya

Aidha amemtaka kutekeleza agizo la kuijibu barua aliyomwandikia Mhe. Mkuu wa Mkoa na Mhe. Mkuu Wilaya akimshukuru kumrudishia eneo lake na nakala ampatie Mkurugenzi  ikiwa ni pamoja na kuwaomba msamaha viongozi kwa kuwa aliwadanganya.

“Tukiruhusu viongozi wetu ambao Mhe. Rais anawateua  watumike vibaya sababu ya ujuaji hatuwezi kufika mbali na kwa vile nimeona umuhimu wa hili tuna viongozi wa TAKUKURU hapa na OCD ametuma watu wawili hili suala lisipo tekelezwa Mwanasheria mchukue hatua wizi wa mabati,matofali, uvunjaji wa becon na miti tuliyoilipia ikachukuliwa virejeshwe hapa,”amesisitiza Mkurugenzi Sweya

Akiongea Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mhe. Mohamed Kiberenge amesema maagizo ya Mkurugenzi yatekelezwa sababu ni agizo la kiutendaji na kuwataka waliokuwa wakilalamika wkatekeleze maagizo na mambo mengine ambayo yapo kisheria yakaendelee.

“Naomba sasa hili lifike mwisho na mradi uendelee kama tulivyokubaliana na hii ni kamati ya fedha ambayo inasimamia mali za Halmashauri kwa kushirikiana wataalam na madiwani kwa hiyo niwaombe sasa nyie mna nafasi ya kuzungumza na wanasheria kwa sababu sisi ni vyombo vinasimama na nyie hatuna muda wa kusikiliza kesi tena kwasababu tulisha maliza na kuwalipa fidia kwa hiyo mtaendelea kukiri kwenye vyombo,”amesisitiza Mhe. Kiberenge.

Ndg. Fonga ni mmoja wa wananchi waliolipwa fidia ili kupisha eneo kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Bicha na viwanja ambapo alilipwa shilingi milioni 40 ikiwa ni kwa ajili ya eneo, makaburi, miti na gharama za usumbufu ambapo amerudi na kujenga katika eneo hilo kinyume na taratibu za fidia.A

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa