• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Baraza la Madiwani lapongeza utendajikazi wa pamoja

Tarehe iliyowekwa: January 29th, 2025

Baraza la Waheshimiwa Madiwani katika Halmashauri ya Mji Kondoa wamepongeza utendaji kazi wa Mkurugenzi na watumishi wake katika ngazi zote hali inayopelekea mambo mengi kufanyika kwa wakati na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge wakati wa baraza la kata la kujadili taarifa za kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025 lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

“Mkurugenzi umerudisha moyo wa utendaji kazi kwa watumishi tunakupongeza sana japokuwa wapo wachache wanahitaji kuendelea kubadilishwa lakini mnafanya kazi nzuri tumeona hata kwenye upitishaji wa bajeti mlivyofanya imekuwa shirikishi katika vikao vyote vya kisheria imejenga uelewa wa Pamoja wa wajumbe wote,”amesema Mhe. Kiberenge

Ameongeza kwa kusema kuwa waendeleze umoja wao kwa kuhakikisha wanawashirikisha kwa ukaribu zaidi watendaji katika katika kazi ya ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa.

Aidha ameshauri kuendelea kufuatilia kibali cha ajira katika mamlaka za juu kwa lengo la kupata watendaji ambao watasaidia katika kuboresha utendaji kazi na kuipaisha halmashauri katika Nyanja tofauti.

Pia amepongeza matokeo ya kidato cha nne na pili kwa shule zilizofanya vizuri na kushauri kuendelea kuwa karibu na wanafunzi kwa ajili ya kuongeza GPA jambo ambalo litafanikiwa iwapo wahusika wote watashirikiana.

“Mkurugenzi katika kata ya Kilimani na kata zingine kuna maeneo ya wazi ya Halmashauri baadhi ya watu wamejimilikisha tunaomba yafuatiliwe na tunaomba katika maeneo ambayo yamepimwa watu wasijenge kiholela wafuate taratibu zote za kisheria,”amesema Mwenyekiti Kiberenge

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amewashukuru Waheshimiwa madiwani kwa pongezi walizozitoa ambapo amesema wataendelea kudumisha umoja huu kwa kuhakikisha unajenga familia moja na kuifanya Halmashauri kuwa na sifa za kuwa Manispaa.

“Kuhusu suala la kibali cha watumishi tutaendelea kufuatilia ambapo kwasasa tunaendelea kuhakikisha maeneo ambayo hakuna watendaji tunapambana kuajili kwa mkataba ili kazi zisikwame lakini pia niwashauri watendaji wa kata penye changamoto toeni taarifa wakati wowote ili tuweze kuhakikisha wananchi wanapata huduma,”amesema Mkurugenzi Majaliwa

Baraza la Madiwani la kazi limefanyika kwaajili ya  kujadili taarifa za utendaji kazi kwa robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka katika kata zote 8 za Halmashauri na limehudhuriwa na Kamati ya Usalama, Wakuu wa Idara na vitengo pamoja na Maafisa Tarafa za Kondoa Mjini na Kolo.

 

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Chuo Kikuu Mzumbe watoa elimu sheria za mazingira kwa Watendaji Kondoa Mji

    June 13, 2025
  • Kondoa Mji wapongezwa kupata hati safi kwa mwaka 2023/2024

    June 10, 2025
  • "Sintamzibia ruhusa mtumishi anayetaka kwenda masomoni"- Mkurugenzi Majaliwa

    June 01, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa