• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bilioni 2.2 kutengeneza barabara saba na daraja moja Kondoa

Tarehe iliyowekwa: October 25th, 2022

Ofisi ya TARURA Wilaya ya Kondoa mbioni kuanza kutengeneza barabara saba na daraja moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.2 ikiwa ni miradi ya awamu ya kwanza kupata fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TARURA Wilaya ya Kondoa Mhandisi Daudi Sweke wakati wa hafla ya kuwatambulisha wakandarasi sita watakaoanza kufanya kazi za kutengengeneza barabara iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa.

Akiongea katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amewataka wakandarasi hao kuongozana na wahandisi wa Halmashauri na Maaifa Tarafa kwenda kutambulisha miradi hiyo kwa wananchi ili wajue thamani, ukubwa wa barabara na muda wa utekelezaji wa mradi na kuachana na tabia ya kwenda kwa viongozi wa vijiji na mitaa wapatapo matatizo.

“Siyo pale unapokuwa umekwama hapana kutoka mwanzo unapoenda kwenda kwa mtu gonga hodi sidani kama inakupunguzia chochote kwa hiyo ni vyema kama kata na tarafa mkawatambulishe kule na kama kuna kitu kule ambacho kinahitajika kwa wananchi wanatakiwa wakifanye sisi tunapaswa tuwasemee wakandarasi kwa wananchi,”amesema Dkt. Mkanachi

Aidha amesema moja ya kazi ya jeshi la akiba ni kulinda miundombinu ya maeneo yenye miradi hii na jamii husika hivyo waelekezwe kuwa kuna mradi ikiwa ni pamoja na kumjua mkandarasi ili iwapo litatokea jambo lolote wajue wanatoa taarifa kwa nani kwa kuwa kuna baadhi ya wananchi huujumu mali za wakandarasi.

“Niwaombeni wakandarasi watu mnaowaleta kufanya kazi au kusimamia kazi wawe na uchungu na kazi zenu kwa kuwa kuna watu mnawapa kazi ila hawana uchungu na kazi zenu ye anachoangalia nalipwa  na ukumcheleweshea malipo analalamika kwa hiyo tafuta watu ambao kweli wana uchungu na kazi na wenye hamu ya kuona unamaliza kwa wakati,”amesisitiza Dkt Mkanachi

 Akiongea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Mhe. Hija Suru amesema wanatarajia makubwa kupitia wakandarasi hao kwa kuwa ana imani hadi wamepata kazi hiyo wamepitia michakato mirefu hivyo wazingatie viwango vinazingatiwa na hawatavumilia kuona wananchi hawapati wanachostahili na kuwataka kukumbuka kuweka alama za michepuko panapostahili ili kuepusha ajali zisizo na ulazima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amewataka wakandarasi watakaotekeleza mradi Kondoa Mji kuutekeleza kwa kuwa ni mradi wa kimkakati kwa kuwa unapita katika eneo linapopita bomba la mafuta ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mhe. Maguo Abdala amesema barabara huchochea maendeleo hivyo ujio wao ni mzuri pia akawaasa kushirikisha halmashashauri nzima ya kijiji na si wenyeviti peke yao ikiwa ni pamoja na kuwataka kuacha kufanya biasahara yam awe kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kazi zao.

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Annette Nara amewaomba wakandarasi kutoa ushirikiano kwa wananchi na taasis kama shule za sekondari na msingi wanapowafuata kuomba mahitaji wasisite kuwasaidia.

Akiongea kwa niaba ya wakandarasi Ndg. Godiozo Tuyanywe amesema anawashukuru viongozi kwa maneno mazuri na wanahaidi kufanya kazi kwa wakati na kwa kuzingatia viwango ili thamani ya fedha iweze kupatikana kwa kuwa nia ni kusaidiana pande zote mbili.

Jumla ya miradi ya wakandarasi 7 wametambulishwa ambao watajenga barabara tano ambazo zitatengenezwa Kondoa  Vijijini  ni Thawi-Kwadinu, Kikore-Hurui, Intera-Nsolo,Pahi-Haubi na Unkuku-Loo aidha barabara zingine ni za kufanyia matengenezo ya kawaida sehemu korofi na muda maalum ambapo barabara zitakazotengenezwa ni Mkunduru-Kisaki,Itundwi-Bumbuta, Itaswi-Mahongo,Ntundwa-Hurui na Kinyasi Majengo-Itaswi-Chubi na Bereko- Kisese-Dachenche, Kisese-Kikore, Mapinduzi-Disa daraja moja ni raraja la Hurui kwa Kondoa Mji ni barabara ya Msui-Kingale-Serya na Munguri Swagaswaga ambapo barabara zote hizi zitatengenezwa kwa kiwango cha lami.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa