• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bilioni 49.4 zatolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilaya ya Kondoa

Tarehe iliyowekwa: February 20th, 2024

Zaidi ya bilioni 49.4 zimetolewa na serikali kuu, wadau wa maendeleo na wafadhili zimetolewa kwaajili ya utekelezaji wa maendeleo kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2023.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha nusu mwaka mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama katika Ukumbi wa CCM.

"Mhe Mwenyekiti fedha zilizoletwa na Serikali ni nyingi shukrani za dhati kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha zote hizo na kutuamini tuliopewa dhamana na tutaendelea kuzisimamia fedha hizo kwa uaminifu" amesema Dkt. Mkanachi 

Aidha ameongeza kuwa fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji miradi katika sekta za elimu, afya, barabara, maji na nishati ambazo zimelenga kuwasaidia wananchi kupata huduma.

"Katika sekta ya afya zimetolewa milioni 60 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati lakini pia milioni 400 kwajili ya ununuzi wa dawa pamoja na bilioni 1.4 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na kwasasa upasuaji unafanyika Kondoa hakuna haja ya kwenda Dodoma,"amesisitiza  Dkt. Mkanachi

Ameongeza kuwa kwa upande wa elimu serikali imeleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kisasa nyumba za walimu na shule mpya mbili za msingi zilizokamilika na zinatumika kwasasa.

"Kwa upande wa nishati serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya kusambaza umeme na kuongeza nguvu ya umeme ambapo kati ya vitongoji 381 vya wilaya ya Kondoa vitongoji 217 vinapata umeme ambapo tuna uhakika hadi mwaka huu wilaya nzima itakuwa inapata huduma ya umeme" amesema Dkt. Mkanachi

Hata hivyo amewashukuru wabunge wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ambaye ni mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Ally Makoa mbunge wa Kondoa Mjini kwa kuhakikisha fedha hizo zinakuja Wilayani kwa ajili ya wananchi wao.

Wakiongea kwa upande wao wajumbe wa kikao hicho wamempongeza Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa uwasilishaji wa taarifa hiyo na kumuomba kusaidia kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya afya ikiwemo upungufu wa watumishi.

Kikao cha Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kimefanyika kwa ajili ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2023.


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa