• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bilioni 8 zatumika kutatua changamoto za wananchi Kondoa Mjini

Tarehe iliyowekwa: August 2nd, 2024

Shilingi bilioni 8 zilizotolewa na Serikali kuu, wafadhili mapato ya ndani ya Halmashauri na mfuko wa jimbo zimetumika katika kutatua changamoto katika sekta za elimu, maji, barabara, biashara na umeme zilizokuwa zikiwakabili wananchi wa kata ya Kondoa Mjini katika Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kipindi cha miaka minne.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge alipokuwa akiongea kwenye mkutano wa hadhara wa kutangaza fedha za miradi zilizoletwa katika kata ya Kondoa Mjini uliofanyika katika viwanja vya Stendi ya Zamani.

“Hizi fedha zilizotolewa ni za Kondoa Mjini peke yake na kila kata imepewa mgao wake na nipo tayari kuelezea kila fedha iliyotolewa na kazi iliyofanya lakini nyie ni mashahidi mnakumbuka kulikuwa na mrundikano wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Maji ya Shamba lakini serikali sikivu ikatusaidia tukajengewa shule mpya ya Msingi Migungani na kuondoa tatizo la mrundikano kwa wanafunzi,”amesema Mhe. Kiberenge

Ameendelea kueleza kuwa pia serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa sgule mpya ya Sekondari Tura Day ambapo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza umbali wa kutembea wanafunzi wanaomaliza Shule ya Msingi Mpalangwi na Kichangani.

“Nyie mashahidi fedha hizo zimejenga madarasa 10 Ula sekondari na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 45 hadi asilimia 95, madarasa 12 Miningani na matundu ya vyoo, madarasa 6 Shule ya Msingi Mpalangwi, madarasa 4 Tumbelo ikiwa ni pamoja na kuongeza madarasa Shule ya Msingi Serengeni ambayo kwasasa imesajiliwa na kuwa shule kamili,”amesisitiza Mhe. Kiberenge

Kwa upande wa barabara amesema Serikali imetoa fedha kwajili ya kuunganisha mawasiliano kati ya Thawi na kata za Kondoa Mjini na barabara ya Iboni Gubali imeboreshwa ili iweze kupitika muda wote kwa lengo la kuongeza fursa za kujipatia kipato kwa kupitisha biasahara muda wote na kupunguza gharama za usafiri.

Aidha amempongeza mbunge wa Kondoa Mjini Mhe. Ally Makoa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile kwa kuwapambania wananchi wa Kondoa Mjini na kupunguza tatizo la maji kwa kiasi kikubwa na kuwaombea wananchi wa Kichangani waruhusiwe kuvuta maji majumbani kwao.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi kata ya Kondoa Mjini Ndg. Samson Mtui amesema fedha zilizopokelewa  shilingi bilioni 2.5 kwa miradi ya elimu, shilingi milioni 26.7 mfuko wa jimbo, shilingi milioni 25 mapato ya ndani, shilingi milioni 172 vikundi vya wanawake,vijana na walemavu, mradi wa maji bilioni 4.5 na barabara shilingi bilioni 1.3 na kufanya kata Kondoa Mjini kuwa na miradi yenye gharama ya shilingi  bilioni 8.

Kwa upande wa wananchi wameomba kupatiwa msamaha wa kodi ya majengo hasa wazee wasiojiweza na kuomba kupunguziwa gharama za kuingiza umeme kutoka shilingi laki 3 hadi shilingi elfu 27 kwa kuwa wananchi hao wanakipato cha chini.

Kata ya Kondoa Mjini  inaundwa na mitaa 6 yenye wakazi 26179 ambapo wanaume ni 12675 na wanawake 13504 kwa sensa ya mwaka 2022 na zaidi ya asilimia 90% ya wakazi ni wafanyabiashara na Mwenyekiti amefanya mkutano huo ikiwa ni kata ya tatu kati ya 8 ambapo anaambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri naTaasis zingine za Serikali.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa