• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Caren akawe chachu katika michezo mashuleni"- Mkurugenzi Dakawa

Tarehe iliyowekwa: August 27th, 2019

Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kumtumia mwanafunzi Caren kama mfano wa kuigwa katika michezo ili kuibua vipaji zaidi katika shule zao.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi walifanya vizuri katika ngazi ya taifa na Afrika Mashariki hivi karibuni.

“Wakuu wa shule endeleeni kuwapa nafasi wanafunzi katika michezo ili kuibua vipaji tofauti vya michezo mashuleni ikiwa ni pamoja na kuwapa nafasi walimu wa michezo kuonyesha uwezo wao na kuzalisha vipaji zaidi kwasasa michezo ni ajira.” Alisema Mkurugenzi Dakawa

Aliongeza kwa kuwapa moyo wanafunzi walioshinda kuendelea na jitihada hizo na kuendelea kutumia fursa wanazozipata kuonyesha kuwa wanaweza kwani ukiamini katika kuweza unafikia malengo uliyojiwekea.

“Nawapongeza wote walioshiriki katika michezo tofauti na Caren aliyeng’ara katika michezo ya Afrika Mashariki shule iendelee kumuunga mkono katika juhudi zake ili aweze kuendelea kung’ara zaidi na kufika mbali kwani kitaaluma pia.”Alisisitiza Mkurugenzi Dakawa.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Pancracy Meleko aliwapongeza wanafunzi hao na kumpongeza Mkuu wa Shule ya Wasichana Kondoa kwa kuonyesha moyo wa kuwaunga mkono wanafunzi katika michezo na kuzalisha kipaji cha wanafunzi Caren.

“Nimewaita na Wakuu wa Shule zote ili mkawe chachu katika kuinua michezo na kwasasa dunia imemuona Caren ambaye anacheza michezo yote na anafanya vizuru kitaaluma hivyo tukaibue vipaji kama hivyo.”Alisema Mwalimu Meleko.

Aidha aliongeza kuwa Halmashauri kwa kuunga mkono jitihada zao itamzawadia mwanafunzi Caren kwa kumlipia ada yote ya kidato cha sita, kumpatia cheti cha ukumbusho na kumlipia ada ya likizo ya mwezi Desemba na wanafunzi wengine watapewa sare za shule na madaftari ya mwaka mzima.

Akiongea mwanafunzi Caren Molel alisema kuwa watanzania wanaweza kufanya vizuri katika michezo kikubwa ni wazazi kuwapa nafasi watoto wao ili waonyeshe vipaji kwani michezo ni ajira kwasasa.

Hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika UMISETA taifa na Afrika Mashariki iliyowakilishwa na mwanafunzi Caren ambaye amerudi na medali ya dhahabu na fedha pamoja na kuwa anacheza michezo yote ilihudhuriwa pia na wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Mji Kondoa.  

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa