• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Chandimo watakiwa kushirikiana na kamati ya ujenzi wa madarasa

Tarehe iliyowekwa: May 5th, 2021

Wananchi wa mtaa wa Chandimo wameshauriwa kushirikiana na kamati ya ujenzi katika shule ya Msingi Chandimo na viongozi wa mtaa ili kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na vyoo baada ya kupata shilingi milioni 44 kutoka serikali kuu.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakati wa mkutano wa hadhara wa uhamasishaji wa utekelezaji wa miradi na wananchi wa Mtaa wa Chandimo uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Chandimo.

"Tushirikiane na kamati hizi mlizozichagua wenyewe ili zifanye kazi iliyokusudiwa na wamalize kwa wakati na asitokee mtu yoyote awe kiongozi au mwananchi na kuwatoa katika kazi zao kwa kuwa wamechaguliwa kidemokrasia na tunaamini mnawaamini sababu ni waadilifu ba waaminifu",amesema Mkurugenzi Dakawa 

Aidha ameongeza kuwasihi wazazi kuwasomesha watoto wao ili wawasaidie baadae na kuachana na tabia ya kuwaoza watoto katika umri mdogo kwani kwa kufanya hivyo wanatenda ukatili kisheria kwa kumnyima mtoto haki zake kimsingi na kuahidi kuwachukulia hatua wananchi wote watakaobainika kuafanya hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya usalama.

"Shule hii mna bahati kweli mwaka jana mlipata mradi wa nyumba ya mwalimu na madarasa mwaka huu tena mmepata madarasa mawili na matundu manne ya vyoo kwa kuwa mnajitoa katika shughuli za maendeleo mnaanza wenyewe kutokana na juhudi hizo serikali wanawaunga mkono endeleeni msikate tamaa maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe mtafika mbali," amesisitiza Mkurugenzi Dakawa 

Aidha Mkurugenzi ameagiza walimu wote wa Shule ya Msingi Chandimo kukaa shule ilipo kwa kuwa serikali ilijenga nyumba na kuahidi kuwachukulia hatua walimu wote watakaokaidi agizo hilo ili watoto wasome wakati wote.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Irene Mosha aliwataka wananchi kwa kushirikiana na walimu kuzuia utoto wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanautumia vizuri chakula walichovuna na kuwasisitiza vijana kuchangamkia fursa za mikopo ili waweze kujiinua kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Chandimo Shabani Issa amemshukuru Mkurugenzi kwa kufika katika eneo Lao na kuwapa moyo na kusema kuwa wananchi wa Chandimo wanajituma siku zote na ni wasikivu hivyo anaamini fedha zitatumika ilivyokusudiwa na kwa wakati.

"Vijana tujitume kwenye kazi za maendeleo na ni neema kubwa kwetu kupata miradi mingi hivi na hii nina imani kwa kuwa wengi huwa mnajitoa ikija miradi mnaishughulikia inakamilika kwa wakati tuendelee na moyo huo huo," amesema Mwenyekiti Shabani

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chandimo Maulid Issa amemuomba Mkurugenzi kuongezwa ukubwa kwa kalvati la Dumi ili maji yasisambae maeneo mengine kwa kuwa mvua ikinyesha maji yaliyosambaa yanahatarisha usalama wa wanafunzi wanapokwenda shule.

Ziara ya uhamasishaji utekelezaji wa miradi umefanyika katika Shule ya Msingi Chandimo ambapo imepata fedha kiasi cha shilingi milioni 44 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na matundu manne ya vyoo na katika ziara hiyo alikuwepo Mkurugenzi, Afisa Maendeleo ya Jamii, Mhandisi ujenzi, Afisa Mipango na Afisa Manunuzi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa