• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Chanjo ya UVIKO 19 ni hiari yenye umuhimu

Tarehe iliyowekwa: September 24th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt.Khamis Mkanachi amesema chanjo ya UVIKO 19 si lazima ila ni hiari yenye umuhimu mkubwa kutokana na madhara anayoyapata mgonjwa aliyepata maambukizi ya virusi hivyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao kazi cha kuweka mkakati wa uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19 na kamati ya Afya ya Msingi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

"Wengi tumeshuhudia watu wanakufa ugonjwa upo lakini na chanjo ipo na niwakikishie ni salama kabisa niwaombe wataalam wa afya watoke kwenda kwa wananchi kuwafikishia elimu lakini pia kuhakikisha wanachanja ili kuokoa afya zao,"amesema Dkt. Mkanachi

Aidha amesema elimu inapoendelea kutolewa na chanjo iendelee kutolewa kwa kuwa si rahisi watu wote wakachanja kwa wakati mmoja hivyo wapo wataochanja leo na wengine kesho kutokana na kila mtu na mapokeo yake.

"Viongozi tuchanje sisi tunakutana na watu wengi tupo katika makundi hatarishi hivyo tuchanje kwanza sisi tusiishie kuhamasisha tu wengine na viongozi wa dini nawaombeni tuhamasishe watu wetu wachanje gharama za matibabu ni ghali sana,"amesisitiza Dkt. Mkanachi.

Akitoa elimu ya kirusi cha Corona Dkt.Nassoro Matuzya Mratibu wa Elimu ya Afya mkoa wa Dodoma amesema Tanzania ni nchi ya pili Afrika kuwa na kifaa cha kukagua ubora wa chanjo zinazotolewa iwapo zina protein inayohitajika na ndicho kilichotumika kupima chanjo inayotolewa Tanzania na kuthibitishwa ni salama.

"Chanjo ya J & J ndio chanjo pekee ambayo mtu anachoma mara moja tu na imethibitishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni na haina madini yoyote kama inavyosemwa na ilihakikiwa na kamati ya kuchunguza chanjo iliyoundwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema Dkt. Matuzya 

Naye mratibu wa chanjo Halmashauri ya Mji Kondoa Evance John amesema hadi kufikia Sept 23 jumla ya watu 1858 wamechanja katika wilaya ya Kondoa ambapo lengo ni kukamilisha chanjo 7000 zilizoletwa wilayani hivyo kila mtu akatumie elimu iliyotolewa kwa nafasi yake kuhamasisha watu wapate chanjo.

Wakitoa ushuhuda wa chanjo kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kondoa na Padre wa kanisa katoliki Itololo wamesema toka walipochanja hakuna madhara yoyote waliyopata maneno wanayosikia  ni ya watu wasio na nia njema na afya za watu nani maneno ya watu wa mitaani.

Kikao kazi cha Afya ya Msingi kimefanyika kuweka mikakati ya kuhamasisha chanjo ambapo wajumbe wamekubaliana kufikisha chanjo katika maeneo ya masokoni, minadani, mikutano ya hadhara, nyumba za ibada na vyuoni na walengwa watapewa elimu kabla ya kuchanjwa ambapo pia vituo vya kutolea chanjo vimeongezeka na kufikia vituo 45 kwa wilaya yote ya Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa