• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Makota aagiza wanafunzi kupata chakula katika shule zote

Tarehe iliyowekwa: February 10th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota amewaagiza viongozi wa kata na mitaa kuhakikisha kuwa kuanzia Aprili mosi wanafunzi wanapata chakula cha mchana shuleni katika shule zote.

Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni ambapo wadau mbalimbali wa elimu walikusanyika.

"Watoto wapate chakula shuleni na walimu wawezeshwe chai shuleni ili kuokoa muda wa kwenda kunywa chai nje ya shule na haya yanawezekana tukiamua kushirikiana wote," amesema Mhe. Makota.

Aidha amewataka Walimu na Maafisa Elimu Kata kuwajibika na kuzingatia nidhamu kwani ndio nguzo ya kufanya vizuri kwa wanafunzi na kuahidi kuwachukulia hatua walimu wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuacha tabia hiyo mara moja.

"Naomba niwaambie wadau ambao ndio wazazi wa wanafunzi wa watoto wenye mitihani ya kitaifa mwaka huu kuwa makambi kwasasa yatakuwa kwa miezi mitatu yaani baada ya kufungua shule mwezi Julai mwaka huu tunataka kufaulisha na kurudi kwenye ubora wetu hivyo tujiandae," amesisitiza Mhe Makota

Hata hivyo amekabidhi mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika shule za Bolisa, Serya na Tumbelo ikiwa ni mifuko iliyotolewa na ofisi ya CCM mkoa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wilaya kwa upande wa elimu baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi na kuridhishwa na utekelezaji wake.

Akiongea Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa  amewaomba wadau kuelewa kuwa serikali haijakataza kuchangia masuala ya elimu kwa hiari ila imekataza kuwalazimisha wananchi kuchangia kwa nguvu.

"Walimu nawaasa kuachana na wanafunzi si wake zenu hao wazazi wamewaleta shuleni kusoma si kuolewa na mjue mkijihusisha nso kimapenzi hawezi kuelewa unapomfundisha na chukulia huyo kama mwanao tunataka yote haya yakome ili wanafunzi wafanye vizuri na kuinua elimu wilayani," amesisitiza Mkurugenzi Dakawa

Akichangia wakati wa kikao hicho mzee Kova amewasihi wadau wa elimu kushirikiana kwa kufanya kutekeleza maazimio kwa pamoja na kusisitiza wazazi kuchangia chakula shuleni ili watoto wale kwani ni vigumu kwao kuelewa wanapokuwa na njaa.

Kikao cha wadau wa elimu kimefanyika kwa lengo la kupitia utekelezaji wa maazimio ya mwaka jana na kuweka mikakati ya kuongeza kiwango cha ufaulu na uboreshaji wa hali ya elimu ndani ya wilaya ambapo kilihudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama, viongozi wa dini, walimu, wanafunzi wawakilishi, wakuu wa Idara, wenyeviti wa mitaa na watendaji wa kata na mitaa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa