• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC MAKOTA: “Viongozi wa Elimu Kondoa wajibikeni katika kazi zenu”

Tarehe iliyowekwa: December 17th, 2019

Maafisa Elimu katika Halmashauri za wilaya ya Kondoa, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu katika Wilaya ya Kondoa wametakiwa kuwajibika kwa kazi walizoajiliwa nazo ili kuboresha elimu wilayani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota katika kikao cha kujadili hali ya ufaulu katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2019 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Maafisa elimu mliopo halmashauri muwajali na kuwapenda walimu kwa kuhakikisha kuwa wanapata posho zao, likizo zao na kuwapandisha vyeo kwa wakati ili wawe na moyo wa kupenda kufundisha kutokana na mazingira yao,” alisema Mhe. Makota.

Aidha aliwataka baadhi ya watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuwaagiza Maafisa Elimu ngazi ya wilaya kuacha kukaa maofisini na badala yake wakafanye ukaguzi mashuleni kwani kwa kufanya hivyo hupelekea walimu kuwajibika.

“Mimi sifurahii hata kidogo kuanguka kwa Kondoa najisikia fahari ninapoona tunaongoza na napenda kufanyakazi na watu wanaowajibika na kupenda kufanyakazi kwani mafanikio yanapopatikana ni ya wote na si Mkuu wa Wilaya peke yake,”alisisitiza Mhe. Makota.

Hata hivyo alisikitishwa na baadhi ya changamoto zilizotolewa na wataalam wa Idara ya Elimu kuwa kushuka kwa ufaulu kumechangiwa na utoro na kutokujua kusoma na kuandika kwa wanafunzi ikiwa wao kama viongozi wapo hapo ili kuyadhibiti hayo hivyo akawataka kujipanga na kujirekebisha upya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa aliwataka viongozi hao kuwatia moyo walimu kwani wanafanya kazi katika mazingira magumu  na kwa kufanya hivyo watafarijika na kuona wanawajali.

“Serikali ya awamu tano imejitahidi sana kuhakikisha stahiki za walimu zinapatikana ikiwemo kuwapandisha walimu madaraja, kutoa fedha za likizo na kuboresha mazingira ya kufundishia kikubwa ni kuhakikisha kila mmoja anawajibika ili kufikia malengo,”alisema Mkurugenzi Dakawa.

Kikao cha tathmini ya matokeo ya matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2019 kiliandaliwa na Mkuu wa Wilaya na kilihudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Maafisa Elimu ngazi ya Wilaya, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa shule zote za Msingi ndani ya Wilaya ya Kondoa. 

   

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa