• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Mkanachi awapongeza watoa huduma Zahanati ya Kichangani

Tarehe iliyowekwa: March 20th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amewapongeza waoa huduma katika Zahanati ya Kichangani kwa namna wanavyotoa huduma kwa wananchi wengi kwa mwezi pamoja na uchache wao.

Pongezi hizo amezitoa alipofanya ziara katika kituo hicho kujionea hali ya utoaji huduma katika kituo hicho ambapo pia alitembelea kituo cha Afya Kingale na Zahanati ya Tampori hivi karibuni.

“Kuhudumia watu 700 kwa mwezi ni wengi sana hongereni sana inaonekana ni jinsi gani huduma zenu zinakubalika na kuaminika na wananchi maana ingekuwa tofauti wasingekuja hapa kwa kuwa zahanati ipo mbali na makazi ya watu endeleeni kutoa huduma kwa wananchi”amesema DC Mkanachi

Ameongeza kwa kuwataka wananchi wanaovamia maeneo ya zahanati kuacha mara moja na kumtaka Afisa Tarafa wa Kondoa Mjini Ndg. Ally Mbena kuonana na wananchi hao ili kujua sababu za kuvamia eneo hilo na kutafuta suluhu ya pamoja na eneo la zahanati kubaki salama.

Akisoma taarifa Mganga Mfawidhi wa ya zahanati Ngd. Husna Mlay ameiomba serikali kuwaongezea majengo ya kutolea huduma na kuongezewa watumishi pamoja na nyumba ya watumishi kumaliziwa ili watoa huduma wakae karibu na kituo na kutoa huduma wakati wote.

“Kituo chetu kinatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje, wagonjwa wa msamaha hasa wazee wenye vitambulisho vya matibabu ya bure na wananchi wasio na uwezo wenye vibali na huduma ya mama na mtoto na tunapokea wagonjwa pia kutoka nje ya mtaa huu wa Kichangani,”amesema Mganga Mfawidhi.

Akiongea katika Zahanati ya Mulua ambayo ipo hatua za ukamilishaji baada ya kupokea shilingi milioni 25 kutoka Serikali Kuu amewataka wataalam wa Halmashauri kufanya kazi kwa kushirikiana hasa idara zote zinazohusika ili kuhakikisha taratibu za manunuzi zinafanyika kwa wakati na kazi ya umaliziaji kuendelea ili zahanati ianze kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.

Ziara ya Mkuu wa Wilaya imefanyika kwa lengo la kujionea changamoto za vituo vya kutolea huduma ambapo pia ametembelea katika Kituo cha Afya Kingale,Zahanati ya Tampori na zahanati ya Mlua iliyopo katika ujenzi na mnada wa Bicha ameongozana na Wakuu wa Divisheni na vitengo kutoka Halmashauri ya Mji.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa