• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Nyangasa ataka maoni ya dira ya taifa 2050 yalenge maslahi ya wengi

Tarehe iliyowekwa: August 31st, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa aewataka wajumbe waliohudhuria  kikao cha dharula cha  Kamati ya Ushauri Wilaya kilicholenga utoaji maoni juu ya dira ya Maendeleo ya Taifa kwa miaka 25 yaani 2025 hadi 2050 kutoa maoni yao kwa kuzingatia maslahi ya wengi ambao hawajapata nafasi ya kuhudhuria kikao hicho.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha kukusanya maoni ya dira ya 2050 kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi ambapo kimehudhuriwa na wadau mbalimbali ambao ni Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, Wakuu wa Idara na Vitengo, wafanyabiashara, viongozi wa dini, watu wenye mahitaji maalum, vongozi wa vyama vya siasa, wakulima na wafugaji, watendaji wa kata na Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu.

Akiongea katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya amesema Kondoa ya sasa ni tofauti na ya miaka mingi nyuma hivyo wajumbe watoe maoni ambayo yatasaidia kutengeneza Kondoa waitakayo miaka 25 ijayo ambayo pia itasaidia wilaya na nchi kwa ujumla kukua kiuchumi kwa kuzingatia hali ya vipato pia.

“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeandaa kikao hiki kwa lengo la kupokea maoni kuhusu; Dira ya Maendeleo ya Taifa ambayo inakamilika muda wake mwaka 2025 ambayo ilianza kutekelezwa mwaka 2000 pamoja na kutoa maoni ya Dira ya Maendeleo ya miaka 25 ijayo (hadi kufikia mwaka 2050) ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kupitia Tume ya Mipango inaendelea kukusanya maoni  chini ya Kauli mbiu “Shiriki katika Kuijenga Tanzania Tuitakayo Ifikapo 2050,”amesema Mhe. Fatma.

Ameendelea kueleza kuwa  maandalizi ya Dira ya Maendeleo 2050 hayana budi kuungwa mkono na wananchi wote, ndiyo maana katika kuiandaa, Serikali inakusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili Dira hiyo iweze kupata ridhaa ya wananchi wengi kutoka sehemu zote za jamii yetu  ili Tanzania ya baadae iwe imetokana na maoni ya watanzania wenyewe.

Akitoa maoni yake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amesema kwa kazi kubwa ambayo serikali inafanya ya kuboresha miundombinu anatamani kwa miaka 25 iyajo kusiwe na tatizo la upungufu wa walimu na kuwe na vituo vya afya kila kata pamoja na kazi kubwa iliyofanyika kwasasa ambapo kila tarafa ina kituo cha Afya.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kondoa Mhe.Hija Sulu ameshauri kwa miaka 25 ijayo serikali ione namna bora ya kuwawezesha Wenyeviti wa mitaa kuhakikisha wanapata posho kila mwezi ili kuwawezesha kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayoletwa katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuawezesha wafanyabiashara ndogondogo kupata mikopo itakayosaidia kukuza biashara zao.

Aidha kwa upande wake Afisa Uhamiaji wilaya ya Kondoa Ndg. Mustafa Kipingu ametaka kufikia mwaka 2050 wananchi waendelee kupewa elimu ya kuwa na vitambulisho vya taifa wakati wote na si kusubiria kuvifuatilia wanapokuwa na matukio maalum au kutatua shida fulani.

Akiongea awali mtakwimu kutoka Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Regina Howay amesema pamoja na wadau hao kutoa maoni hayo pia maoni yanakusanywa kupitia madodoso waliyoyatoa katika kikao na tovuti ya tume ili kupata maoni kutoka kwa kila mwananchi.

Kikao cha kukusanya maoni ya uandaaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kimefanyika ikiwa ni sehemu ya hatua iliyopangwa ya kuhakikisha maoni yanakusanywa ngazi zote na mpango huu ulizinduliwa mwaka 2023 na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ikiwa ni maandalizi ya dira hiyo ambapo dira ya mwisho iliandaliwa mwaka 2000 na inatarajia kuisha muda wake mwaka 2025.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa