• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Fanyeni kazi mjiletee maendeleo" - Mkurugenzi Kondoa Mji

Tarehe iliyowekwa: February 13th, 2020

Wananchi wa Mtaa wa Chemchem katika kata ya Chemchem Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kufanyakazi na kujiletea maendeleo ya Mtaa huo kwani maendeleo ya Mtaa huo yataletwa na wananchi wenyewe na serikali ikitekeleza miradi mikubwa.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakati wa mkutano wa mtaa huo wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Kata ya Chemchem hivi karibuni.

“Maendeleo ya Kondoa yataletwa na wanakondoa wenyewe na maendeleo ni gharama yanahitaji kujitoa kuanzia ngazi ya mtaa hivyo mkae na viongozi wenu muone jinsi ya kuongeza vyanzo vya mapato ya mtaa ili muweze kufanya maendeleo makubwa katika mtaa wenu,”alisema Mkurugenzi Dakawa.

Aliongeza kwa kuwashauri wananchi kushirikiana na viongozi wa Mtaa huo kwani kwa kufanya hivyo amani itapatikana na kupata maendeleo.

“Mapato yote yanaingia Halmashauri ila baadaye hugawanywa kwa mujibu wa Sheria na katika mgawanyo huo kuna asilimia 20 ambayo huwa inakuja katika mitaa yenu lakini kwa kuwa makusanyo ni madogo na mgao huwa mdogo ambapo fedha hizo ndizo zinasaidia katika kununua vitendeakazi vya ofisi sasa ili tupate mgao mkubwa tuongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ili tufanye mambo makubwa zaidi,”alisisitiza Mkurugenzi Dakawa.

Akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji wa Kondoa Mhe. Hamza Mafita aliwapongeza viongozi wa Mtaa kwa kuchaguliwa na kumshauri Mwenyekiti wa Mtaa wa Chemchem kuwapangia kazi za kufanya wajumbe wa serikali ya Mtaa waliochaguliwa ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Mtaa wa Chemchem.

“Kazi mliyopewa viongozi ni ngumu na ya kujitolea hivyo inatakiwa muelewane na kumaliza matatizo yenu na mfike mbali na nakushauri Mwenyekiti kuwaachia watendaji na wajumbe kushughulikia masuala ya fedha ili wewe ubaki kuwa msimamizi wa hawa wote,”alishauri Mhe. Mafita.

Aidha Mhe. Mafita alitoa taarifa ya kuanza kujitegemea kama Halmashauri katika program ya kusaidia kaya maskini TASAF kuanzia mapema mwezi Julai ambapo Halmashauri imetengewa zaidi ya shilingi bilioni 2 na kwasasa inaratibiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

Diwani wa Kata ya Chemchem Mhe. Kipaya Mdachi aliwasihi viongozi na wananchi kuilinda amani na kupendana ikiwa ni pamoja na kuepuka majungu, zaidi washirikiane kufanya kazi kwa pamoja kwani hakuna binadamu aliyekamilika.

Wakitoa kero zao katika nyakati tofauti wananchi wa mtaa huo waliiomba Serikali kuwasaidia kuwatengenezea barabara katika kiwango cha changarawe, kupata maji safi na salama na kuwekewa taa za barabarani katika eneo la barabara ya Magereza hadi Hospitali kwani linahatarisha usalama wao nyakati za usiku.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • "Sintamzibia ruhusa mtumishi anayetaka kwenda masomoni"- Mkurugenzi Majaliwa

    June 01, 2025
  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa