• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

FFARS Yaongeza Kasi Ya Utendaji Kazi KONDOA GIRLS

Tarehe iliyowekwa: April 3rd, 2018

Uwepo wa mfumo wa masuala ya utoaji ripoti za fedha na mahesabu katika Shule ya Wasichana Kondoa umeongeza hali ya utendaji kazi kwa walimu tangu kuanza kutumika kwa mfumo huo mapema Julai mosi 2017.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Shule Mwalimu Khalifa Kinasha alipokuwa akiongea ofisini kwake juu ya hali ya utendaji kazi wa mfumo huo toka ulipoanza kutumika shuleni hapo.

’’Kwa kweli mfumo huu umeongeza uzalendo sana kwa walimu kwani umeturahisishia sana kazi ya kuandaa taarifa za fedha tofauti na awali ambapo ilibidi mhasibu atumie muda mwingi  kuandaa taarifa ya fedha na kusimamisha kazi zingine kwani shuleni hapa tunatumia mwalimu ambapo kwasasa anatumia muda mfupi na kuendelena kazi ya kufundisha.”Alisema Kinasha.

Aliongeza kwa kuipongeza serikali kwa ubunifu wa mfumo huo ambao pia umewafanya waendelee kujifunza kompyuta kwa ukaribu zaidi hali inayowafanya waendane na kasi ya ukuaji wa teknolojia unaoendelea duniani.

Hata hivyo aliishauri serikali kuendelea kubuni mifumo mingine mizuri ili kupunguza tatizo la kuwa na takwimu tofauti na hali halisi mashuleni hasa za walimu na wanafunzi hali ambayo pia itapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro kati yao na viongozi kwani watakuwa na takwimu sawa.

Kwa upande wake Kaimu Mhasibu wa shule Mwalimu Mustafa Nkondokaya aliongeza kuwa kwake mfumo huo umekuwa ni msaada mkubwa sana kwani amekuwa akiandaa taarifa ya fedha kwa umakini na uhakika zaidi tofauti na awali ambapo taarifa zilikuwa zinatofautia wakati wa uandaaji.

Aliendelea kueleza kuwa mfumo pia umemsaidia wakati wa kuandaa malipo kwani hujua chanzo cha fedha moja kwa moja na kumlazimisha kutumia fedha kwa nidhamu kulingana na bajeti iliyopangwa ambapo awali alikuwa akitumia fedha bila kujua chanzo na bila kufuata bajeti na kupelekea shule kutumia fedha nyingi bila sababu.

“Mfumo umenirahisishia kazi pia ya utunzaji wa kumbukumbu za taarifa ya fedha na kunifanya niweze kuangalia salio la benki popote nilipo na kwa wakati wowote hivyo napata muda mwingine wa kuendelea na majukumu mengine ya ufundishaji.” Mustafa

Aidha alifafanua zaidi kuwa uwazi umeongezeka katika masuala ya fedha kwani ngazi mbalimbali wanaweza kuangalia mfumo mzima wa makusanyo na matumizi ambapo awali iliwalazimu kwenda kupeleka taarifa hizo kwa gharama zinapohitajika na hali hii imepunguza ubadhilifu kwa kiasi kikubwa kwa watumishi wasio waaminifu.

Mfumo wa masuala ya utoaji wa ripoti za fedha na mahesabu ulianza kutumika Julai 2017 kwenye zahanati, vituo vya afya, hospitali na mashuleni ili kuboresha masuala ya fedha kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa