• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Hachwi watakiwa kuacha tofauti ujenzi wa Zahanati

Tarehe iliyowekwa: December 23rd, 2020

Wananchi wa mtaa wa Hachwi katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kuacha tofauti zao katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwani kwa kufanya hivyo wanachelewesha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Hassan Kiseto wakati wa mkutano wa wananchi kuhusu ujenzi wa Zahanati ya Mtaa huo uliofanyika katika ofisi za mtaa wa Hachwi hivi karibuni.

"Mradi huu ulitakiwa uwe umeshaanza toka kitambo fedha zipo kwenye akaunti shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hapa lakini ujenzi haujaanza kwa kuwa mnavutana  eneo la kujenga zahanati siyo sawa tunataka kuona kazi inaanza ili lengo la  serikali la kuona huduma zinasogezwa karibu kwa wananchi linatimia," amesema Kiseto

Aidha ameongeza kuwa kwa kuwa wananchi wote wanavutana juu ya eneo la kujenga zahanati ni wazi kuwa wote wanahamu ya kupata maendeleo na kuwaagiza wananchi hao kujenga jengo la Zahanati ilipokuwa zahanati ya awali na wengine kujenga nyumba mbili za watumishi kwa ajili ya kituo cha afya katika eneo lilipo shamba la mtaa.

Akiongea awali diwani wa kata ya Kolo Mhe. Idd Ng'ungu amesema wananchi wa mtaa huo wananeema ya kupata miradi kwani hadi sasa wamepewa miradi minne muhimu kwa mwananchi hao ambayo ni usambazaji wa maji, ujenzi wa madarasa na nyumba ya mwalimu shule shikizi ya Kotumo, ujenzi wa Zahanati ya Hachwi na ufunguzi wa barabara.

Akielezea tatizo lililochelewesha kuanza kwa mradi huo Mtendaji wa Mtaa wa Hachwi Judith Mkumbwa amesema mvutano ulianza  baada ya wananchi ya baadhi ya wananchi kutaka zahanati ijengwe eneo la shamba la wananchi na kupelekea wananchi kuanza kusita kuchangia mchango wa shilingi elfu 10 waliokubaliana.

Kwa upande wao akina mama na baadhi ya wananchi wameomba Zahanati ijengwe ilipokuwa zahanati ya awali kwa lengo la  kuhakikisha wananchi wa maeneo yote ya mtaa wa Hachwi wanafika kwa urahisi zahanati kwa ajili ya kupata huduma za afya.

"Wakina mama sisi ndio tunaoteseka sana katika zahanati yetu hii ya awali tumekuwa tukipata huduma ya mama na mtoto na hapa ni karibu kwa kila mtu lakini kwasasa inatulazimu kukodisha pikipiki hadi hospitali ya wilaya lakini tumeletewa fedha za kujenga zahanati hapa karibu alafu eti tunataka kuipeleka kule mbali tena tutarudisha gharama zilezile za kukodisha pikipiki nashauri mtusaidie ijengwe hapahapa ili kila mtu apate huduma kwa ukaribu,"amesema mmoja wa akina mama.

Mkutano wa uhamasishaji ujenzi wa zahanati ya Hachwi umekuja kwa lengo la kutatua changamoto ya mvutano uliokuwepo awali wa kuchagua eneo la kujenga Zahanati baada ya serikali kutoa shilingi milioni 50 ambapo wataalam mbalimbali wa halmashauri walihudhuria wakiwemo Mwanasheria, Afisa Maendeleo ya Jamii, Kaimu Afisa Mipango, Kaimu Afisa Utumishi, Kaimu Mhandisi, Kaimu Mganga Mkuu na Kaimu Afisa Elimu.


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa