• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Mji Kondoa kusimamia kesi za ukatili wa kijinsia zinazocheleweshwa maamuzi

Tarehe iliyowekwa: December 4th, 2020

Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Kondoa imejipanga kusimamia kesi za ukatili wa kijinsia walizofanyiwa wakazi wa Halmashauri hiyo ili kuhakikisha haki inatendeka kwa waliofanya vitendo hivyo.

Hayo yamesemwa na Bi. Irene Mosha Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wakati wa utoaji elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Bolisa na wananchi wa mtaa wa Msui hivi karibuni.

"Naomba wananchi wote ambao mna kesi za ukatili wa kijinsia ambazo hazijashughulikiwa mziorodheshe na kuziwasilisha ofisini ili nizifikishe polisi kwa ajili ya msaada zaidi lengo ni kukomesha vitendo hivi katika jamii yetu," amesema Irene

Aidha aliwasihi wanafunzi kutoa taarifa kwa walimu wao wakuu au uongozi wa mtaa mara wanapofanyiwa vitendo vya ukatili ili wahusika wachukuliwe hatua kwani huwasababishia maumivu wanafunzi hao na kuwarudisha nyuma kitaaluma.

Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi katika Shule ya Msingi Bolisa Bi. Victoria Mwidunda amesema katika shule yake mwanafunzi mmoja alipigwa na mama yake wa kambo na kupata majeraha ambapo walisaidiana na kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kwasasa anatumikia kifungo gerezani.

Hata hivyo mmoja wa wanafunzi ameshukuru kwa kupatiwa elimu hiyo na kuahidi kutoa elimu kwa watu wengine na kutoa taarifa mara tu watapofanyiwa ukatili ili kukomesha vitendo hivyo.

Utoaji elimu ya ukatili wa kijinsia umefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo Halmashauri imeshirikiana na wadau CCT ambao wametoa elimu na kugawa vipeperushi kwa washiriki waliojitokeza katika kata ya Kingale na Bolisa na mwaka huu kauli mbiu inasema Tupinge ukatili wa kijinsia: Mabadiliko yanaanza na wewe"

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa