• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Mji Kondoa Yajivunia Mafanikio katika sekta zake

Tarehe iliyowekwa: June 5th, 2018

Halmashauri ya Mji Kondoa imejivunia mafanikio waliyoyapata katika sekta zake mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Kilimo, Mfuko wa Maendelo ya Jamii na Mazingira.

Hayo yamebainika wakati wa baraza la kazi lililofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

Akiongea Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Hamza Mafita amesema kuwa kwa upande wa elimu Msingi Halmashauri imeongoza kwa kushika namba moja kwa matokeo ya darasa la saba mwaka 2017 na kupata kikombe ambapo aliahidi kuendelea kuishikilia nafasi hiyo kwa miaka yote kwani nafasi hiyo wanaishikilia kwa mwaka wa pili mfululizo na kuongeza asilimia za ufaulu.

“Katika upande wa elimu Sekondari tumekuwa nafasi ya tatu kimkoa nafasi ambayo hatupaswi kuishikilia kutokana na kuwa na shule chache na tuna uwezo wa kufanya vizuri zaidi lakini tumeshaweka mikakati ya kushika nafasi ya kwanza na naamini tutafanya vizuri sababu tumeshafanya vikao na wazazi, kamati za shule na walimu ambapo tuliweka mkakati wa wanafunzi wote wenye mitihani kukaa hosteli kwa kipindi cha wiki mbili.”Alisema Mhe. Hamza

Aidha aliipongeza kata ya Chemchem kwa kuendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kushika nafasi ya 3 kimkoa ambapo juhudi zimekuwa zikifanywa na Mhe. Diwani wa kata hiyo hivyo ni vizuri walimu na waheshimwa madiwani wengine wakatumia mbinu hizo ili kuinua kiwango cha ufaulu wa shule za halmashauri nzima .

Akiongea kwa upande wa kilimo Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika  Bwana Hassan Kiseto amesema kuwa Halmashauri imeshika nafasi ya kwanza katika uhifadhi wa chakula kwa kutumia teknolojia za kuhifadhi chakula kwa kutumia mifuko maalum na mapipa bila ya kutumia sumu ambapo utafiti uliofanyika umeonyesha wananchi wa Kondoawameelewa kwa kiasi kikubwa teknolojia hiyo.

Akifafanua pia Meneja CHF  Bwana Mwinyikombo Ally amesema kuwa Halmashauri imeongoza kwa mkoa wa Dodoma katika usajili wa wanachama wa CHF ambapo hadi sasa Halmashauri imefikia asilimia 32 na wananchi waliokuwa hai ni asilimia 17 hali iliyopelekea Halmashauri kupata wageni kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo nchini Uswiswi kuja kuulizia mbinu ambazo Halmashauri imefanya hadi kufikia kiwango hicho.

Akiongelea mafanikio katika Idara zingine Mkurugenzi Mji Khalifa Kondo alisema kuwa Halmashauri pia imeshika nafasi ya kwanza kwa usafi wa Mazingira kimkoa na kupewa cheti cha pongezi katika usimamiaji wa bajeti na ufuatiliaji wa miongozo ya matumizi ya fedha za  Afya Halmashauri imekuwa ya tatu kitaifa na ya kwanza kimkoa na kuepelekea kuwa Halmashauri pekee katika mkoa kuongezwa bajeti ya miradi ya afya.

“ Lakinii pia kwenye miradi ya maji mkoa mzima ni Halmashauri pekee iliyoweza kusimamia, kubuni na kuiendesha miradi ya maji, kama mnavyojua katika bajeti ya maji ya mwaka 2017/2018 tulikuwa na shilingi milioni 60 tu lakini kwa ubunifu wetu tumeweza kupata fedha zaidi ya shilingi tatu na miradi inaendelea vizuri na itakamilika kwa wakati” alifafanua Kondo.

Baraza la kazi limefanyika kwa kuwashirikisha wakuu wa Idara, Waheshimiwa madiwani ikiwa ni maandalizi ya kikao cha baraza la madiwani ambapo imeelezwa mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na ushirikiano mzuri kati ya waheshimiwa madiwani na watendaji.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa