• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji wapewa kongole kwa hati safi miaka mitatu mfululizo

Tarehe iliyowekwa: June 19th, 2019

Halmashauri ya Mji wa Kondoa imepongezwa kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kutakiwa kufanya vizuri zaidi ili kutoharibu rekodi hiyo waliyoiweka.

Hayo yalibainishwa na Chami Sasamka Mkaguzi wa Kanda ya Dodoma wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani kwa ajili ya kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Fedha za serikali (CAG) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi.

“Ushirikiano mzuri uliopo baina ya halmashauri yenu na ofisi yetu umepelekea mmepata hati safi na mmepunguza hoja na nina imani ushirikiano uliopo pia katika menejimenti yenu utasaidia kuboresha majibu kwa hoja chache zilizosalia.”Alisema Chami

Hata hivyo aliwashauri viongozi na watendaji wa halmashauri kuendelea kusimamia vizuri halmashauri ili kuwaleta maendeleo ambayo wananchi wanayahitaji na kuendeleza rekodi waliyonayo ya kupata hati safi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji wa Kondoa Mhe. Hamza Mafita aliwapongeza waheshimiwa madiwani na wakuu wa Idara kwa ushirikiano wao ambao umefanikisha kupatikana kwa rekodi hiyo na kuahidi kuendelea kusimamia vizuri ili kuendeleza rekodi hiyo.

Akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa aliishukuru ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa ushauri wao na kuahidi kuendelea kufanyakazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni ili kuepukana na hoja ambazo zimekuwa zikisababisha hasara kwa serikali.

Akiwasilisha taarifa ya Halmashauri kwa niaba ya Mkurugenzi Mweka Hazina wa Halmashauri ya Mji Onesmo Mwonga alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 halmashauri ilikuwa na hoja 30 ambapo baada ya majibu kuwasilishwa na uhakiki kufanyika hoja 10 zilipendekezwa kufungwa na kusalia na hoja 20 ambazo zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na uhakiki utafanyika wakati wa ukaguzi wa mwaka 2018/2019.

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Watumishi watakiwa kuendelea kutoa elimu ya stakabadhi ghalani

    June 23, 2025
  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa