• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji wapongezwa kupata hati safi kwa mwaka 2023/2024

Tarehe iliyowekwa: June 10th, 2025

Halmashauri ya Mji Kondoa imepongezwa kwa kupata hati safi katika ukaguzi wa fedha wa mwaka 2023/2024 na kupelekea Halmashauri kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo jambo ambalo limeipa heshima kubwa Halmashauri na mkoa wa Dodoma kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Ufuatiliaji na Tathmini Ndg. Erick Ntikahela kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani la kupitia na kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

“Mhe Mwenyekiti kila wakati ninaamini haya mafanikio makubwa yametokana na uwepo wa mafanikio  chanya baina yenu Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Halmashauri, viongozi na wadau mbalimbali wa Halmashauri hivyo nawasihi endeleeni kudumisha ushirikiano huo ili kuiwezesha Halmashauri kuendelea kupata hati safi kila mwaka”amesisitiza Erick

Aidha amewataka kuhakikisha hoja zilizobakia zinajibiwa ili ziweze kuhakikiwa na kufungwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yaliyowekwa na Serikali pia kuweka katika vikao vya kisheria agenda ya hoja kuwa ya kudumu ili kuiepusha Halmashauri kuwa na hoja zisizojibika.

Akiongea kwa upande wake Mkaguzi Mkazi wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Karim Mwinyimbegu amelipongeza Baraza la Waheshimiwa Madiwani kwa namna walivyojadili hoja zilizowasilisha na kuipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi na kasi ya utekelezaji wa hoja za ukaguzi zilizoibuliwa kwani zimejibiwa kwa asilimia 55 kiwango ambacho kinaridhisha.

Ameongeza kwa kuishauri Menejimenti kuhakikisha inashirikiana na wakaguzi kuona namna inavyoshughulikia hoja za nyuma badala ya kujibu tu hoja za mwaka husika kwa kuwa ukaguzi mpya huangalia pia hoja za nyuma hivyo kuongeza idadi ya hoja kwa Halmashauri.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amesema suala la kujibu hoja za nyuma limechukuliwa na baraza la Madiwani kwa ajili ya utekelezaji na kuwa hoja zingine ambazo zipo ndani ya uwezo wa Halmashauri zitafanyiwa kazi kwa kipindi kilichobakia na kumpongeza Mkurugenzi kwa kasi nzuri ya kujibu hoja.

Awali akisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mweka Hazina Ndg. Kabengwe Lufulondama amesema Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kipindi cha mwaka wa fedha ilikuwa na hoja 22 zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ambapo majibu yamehakikiwa na hoja 3 zimependekezwa kufutwa na hoja 19 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kwa kipindi cha nyuma ilikuwa na hoja 73 ambapo hoja 51 zimejibiwa na zimependekezwa kufutwa na hoja 22 zipo hatua mbalimbali za utekelezaji.

Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha Sita Kondoa Girls 2025 July 07, 2025
  • Tangazo la kazi za muda June 28, 2025
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji yatoa motisha kwa watumishi waliofanya vizuri ukusanyaji wa mapato 2024/2025

    July 08, 2025
  • Kondoa Mji yatoa milioni 90 ya Mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu awamu ya tatu

    July 01, 2025
  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa