• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji washauriwa kunywa maziwa kuboresha afya

Tarehe iliyowekwa: June 1st, 2021

Na. Leah Joseph

Afisa Mifugo Halmashauri ya Mji Kondoa Bi. Semeni Mwakasege ameiasa jamii kujenga utaratibu wa kunywa maziwa angalau glasi moja kwa siku ili kuboresha afya zao na kujenga jamii imara.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kugawa maziwa na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kunywa maziwa katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya unywaji wa maziwa mashuleni yaliyofanyika katika shule za msingi Kondoa Mji hivi karibuni.

"Maziwa ni muhimu katika mwili wa binadamu kwa kuwa yana virutubisho vingi vinavyohitajika kujenga mwili hivyo mnatakiwa kujenga utaratibu wa kunywa maziwa pamoja na kutumia bidhaa zake ili muweze kuimarisha afya zenu",amesema Bi. Semeni

Aidha ameongeza kwa kutaja faida za maziwa katika mwili wa binadamu kuwa ni pamoja na kujenga misuli, kupunguza uzito, kuongeza hamu ya kula, kulainisha ngozi, kutoa kiungulia na kuondoa msongo wa mawazo.

"Kama tulivyoona faida za unywaji wa maziwa lakini ipo haja ya wafugaji wetu kubadili mtindo wa ufugaji badala ya kufuga mifugo mingi kwa ufahari wajikite katika ufugaji wa kisasa ambapo itasaidia kupata maziwa mengi na kupelekea kuongeza vipato vyao kwa kuyauza katika soko la maziwa", amesisitiza Bi. Semeni.

Halikadhalika Bi. Semeni amesema kuwa licha ya maziwa kuwa muhimu kwa rika zote lakini wameona ni vyema kuanza na watoto ambao ni kundi lililopo katika hatua za ukuaji na kwamba maziwa yana msaada mkubwa katika kuimarisha mifupa na meno na kuahidi kuwa wakati ujao watawafikia watu wengi zaidi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maji ya Shamba Mwalimu Aziza Mtanga amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa kwa kutambua umuhimu wa maziwa kwa wanafunzi na kuwapatia katika maadhimisho hayo na kuahidi kuwa watakuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu juu ya faida za unywaji wa maziwa kwa jamii nzima.

Kilele cha maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa yamefanyika kitaifa Mkoa wa Tanga ambapo Halmashauri ya Mji Kondoa imeshiriki kwa kugawa maziwa kwa wanafunzi zaidi ya mia tatu pamoja na walimu katika shule ya Msingi Ubembeni, Maji ya Shamba na Iboni huku kauli mbiu ikisema " Kunywa Maziwa ya Kwetu Ongeza uzalishaji na Usindikaji".

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa