• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

Tarehe iliyowekwa: June 24th, 2025

Vikundi 16 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu vya Halmashauri ya Mji Kondoa wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuendesha shughuli zao ili wajiinue kiuchumi na kufanya marejesho ya fedha walizopewa.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi ambapo yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa.

"Niwapongeze na kuwaomba muwe wasikivu na kuelewa mtachofundishwa kwa kuwa mmekidhi vigezo na mmepitia michakato mbalimbali hivyo mkafanye vizuri ili mikopo hiyo irudi na kuwanufaisha wengine"amesema Mkurugenzi Majaliwa

Aidha amewasisitiza kutunza nyaraka za vikundi husika ili wakati wa ukaguzi wasipate shida ikiwemo kuwa na ofisi ambayo taarifa zote za kikundi zitapatikana huko badala ya kumuamini mtu mmoja.

Aidha ameongeza kwa kuwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanawapa mbinu za kufanya biashara kulingana na kiwango cha fedha walichopewa ili tija ya fedha hizo zionekane.

"Vikundi viliomba zaidi ya shilingi milioni 300 ambapo Halmashauri imetoa shilingi milioni 90 hivyo wengi mmepata fedha tofauti na mlichoomba hivyo mfanye biashara kulingana na kiwango mlichopewa ili msishindwe kufanya marejesho" amesema Mkurugenzi Majaliwa

Akiongea awali Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halnashauri ya Mji Kondoa Ndg. Wenceslaus Mbilango amesema mikopo inatolewa kwa awamu ya tatu toka iliporejea kutolewa mwaka jana ambapo jumla ya vikundi 16 vimepatiwa shilingi milioni 90.

Nao wanufaika wa mikopo wameishukuru Halmashauri kwa kuwafikiria na kuwapatia mikopo ambayo itakwenda kubadilisha maisha yao kiuchumi na kuahidi kurejesha kama taratibu zilivyo.

Halmashauri ya Mji Kondoa inatoa mikopo kwa awamu ya tatu baada ya kufunguliwa mwezi Oktoba 2024 ambapo zaidi ya shilingi milioni 457 zimetolewa kwa vikundi 54.

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Watumishi watakiwa kuendelea kutoa elimu ya stakabadhi ghalani

    June 23, 2025
  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa