• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KONDOA MJI WAUNGANA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE

Tarehe iliyowekwa: March 8th, 2021

Wanawake wa Halmashauri ya Mji Kondoa wameungana na wanawake wengine nchini na Dunia kwa ujumla katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka.

Sherehe za maadhimisho hayo kwa Halmashauri ya Mji Kondoa zimefanyika siku ya Jumamosi kwa kufanya bonanza la michezo na siku ya kilele tarehe 8 Machi kwa kufanya kongamano katika ukumbi wa CCM ambapo mamia ya wakazi wa mji huo wamehudhuria maadhimisho hayo.

Akiongea katika ukumbi wa CCM Mhe. Zainab Haroub ambaye ni diwani wa Kata ya Chemchem amesema kuwa wanawake wametoka  mbali  kwani tangu kupitishwa kwa mpango wa utekelezaji wa Beijing miaka 25 iliyopita, idadi ya viongozi wanawake imeongezeka, uwepo wa idadi kubwa zaidi ya wanawake kuanzia bungeni, katika taasisi za kiserikali na zisizo  za kiserikali hali ambayo  ina maanisha kuna idadi kubwa ya wanawake watoa maamuzi ambayo yana manufaa kwa jamii naTaifa .

“Haki za msingi za wanawake ni kwa ajili ya watu wote mahali popote pale walipo wadau mbalimbali wanapaswa kuhakikisha kwamba wanalinda na kudumisha haki za msingi za wanawake kwani mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha Miaka 25 iliyopita yanapaswa kuendelezwa na kuboreshwa zaidi sanjari na kuimarisha umoja na mshikamano katika kutetea haki za msingi za wanawake,”amesema Mhe. Zainab

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) uliridhia na kuanza kuadhimisha rasmi Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 1975 kwa lengo la kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia, ambapo uamuzi huu ulifikiwa kupingana na mfumo dume ambao ulitamalaki katika jamii mbalimbali ulimwenguni na kuminya haki za wanawake.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Bi. Lucy Timba akimkaribisha mgeni rasmi amesema licha ya  umoja wa mataifa kutenga siku maalum ya kumuadhimisha mwanamke takribani miaka 100 iliyopita,lakini  bado wanamke anaendelea kunyanyaswa katika baadhi ya mambo ikiwemo fursa za elimu, afya na hata mgawanyo wa kazi katika familia.

Kwa upande wake mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Irene Mosha amewataka wanawake kuzidi kujiamini na kuthubutu kujihusisha na shughuli za kiuchumi ili waweze kujijengea uwezo wa kujitegemea kuliko kumtegemea mwanaume moja kwa moja hali itakayosaidia kupunguza manyanyaso kutoka kwa wanaume wao na jamii kwa ujumla.

Machi 8 kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kutambua nafasi na mchango wa wanawake katika kuchangia maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa duniani na kaulimbiu ya mwaka huu inasema “wanawake katika uongozi chachu kufikia dunia yenye usawa”ambapo katika Halmashauri ya Mji Kondoa iliadhimisha kwa kufanya kongamano lililowakutanisha wanawake na kutolewa kwa mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa huduma za afya.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa