• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji yaanza kutoa huduma ya upimaji udongo kwa wakulima

Tarehe iliyowekwa: September 14th, 2023

Halmashauri ya Mji Kondoa kupitia Divisheni ya Kilimo, mifugo na Uvuvi imeanza kutoa huduma ya kupima udongo katika mashamba ya wakulima bila gharama yoyote lengo likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji kwa wakulima.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo na Mifugo Ndg. Monica Kimario wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake hivi karibuni.

“Utaratibu wa uchukuaji wa sampuli za udongo kwa kata zote nane umeanza mpaka sasa tumechukua udongo katika kata tano ambazo ni Kingale, Serya, Suruke, Kolo na Bolisa ambapo tutaendelea katika kata za Kondoa M,”amesema Ndg. Monica

Amesema kuwa kifaa hicho chenye thamani ya shilingi milioni 11 kimetolewa na Serikali nchi nzima kupitia Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji kwa wakulima ili walime kilimo chenye tija katika eneo dogo kwa kuwa kifaa kitaonyesha kitu gani kimepungua kwenye udongo ili kifanyiwe kazi.

“Zoezi hili ni endelevu hivyo wakulima ambao tumeshapita kwenye kata zao na wanahitaji huduma hii wawaone maafisa ugani wa kata zao ili udongo ukachukuliwe kwenye mashamba yao na watapewa majibu na wale wa kata zilizosalia wajiandae kwa ajili ya zoezi na linafanyika pia kwa taasis ambazo zinajishughulisha na kilimo,”amesema Ndg. Monica

Ameendelea kusema kuwa zoezi la kupima udongo linafanyika katika ofisi za Halmashauri na si shambani wao wanachofanya ni kuchukua udongo na kuja nao ofisini kwa ajili ya vipimo na kuongeza kuwa udongo unaotakiwa kuchukuliwa ni wa kipindi cha kiangazi hivyo wakulima watumie fursa hii kwa kipindi hiki na si wakati wa masika ambapo majibu yanayoweza kupatikana si halisia.

Kwa upande wake Afisa Kilimo Ndg. Hassan Kiseto amesema zoezi hili litasaidia kujua afya ya udongo uliopo, aina ya mazao unayotakiwa kulimwa katika eneo husika, aina ya mbolea itakayotumika na kiasi cha mbolea itakayotumika na kujua kiasi gani cha chokaa kitakachotumika kuongeza uzalishaji.

“Wakulima kipindi cha nyuma walikuwa wakishauriwa kuweka mbolea ya kupandia kwa kipimo maarufu ambacho ni kifuniko cha soda katika shina moja japokuwa  kilisaidia kwa muda mrefu lakini huwezi kujua kama upo sahihi kutokana na ardhi husika,”amesisitiza Ndg. Kiseto

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ambao wamehakikisha bajeti inatengwa na inatekelezwa katika kufanya kilimo kuwa cha kitaalamu na kisasa kwa hatua hii tunadhani tutafikia ukuaji wa kilimo kwa asilimia 10 ifikapo 2030 agenda kuu.

Huduma ya upimaji udongo inatolewa bila gharama yoyote ambapo katika maabara za watu binafsi hupimwa kwa shilingi elfu sabini kwa sampuli moja na kwa shamba moja huchukuliwa sampuli zaidi ya tatu ambayo ni gharama kubwa kwa mkulima hivyo wananchi watumie fursa ya Halmashauri ambapo huduma hii inatolewa bure.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa