• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji Yapongezwa Kwa Ukusanyaji Mapato

Tarehe iliyowekwa: January 30th, 2019

Halmashauri ya Mji wa Kondoa imepongezwa kwa ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kufikia asilimia 67 ya lengo la mwaka na kuwa halmashauri ya 3 kwa halmashauri za miji nchini.

Pongezi hizo zilitolewa na Bwana Peter Gujenji kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

Alisema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatambua na inathamini juhudi zinazofanywa katika ukusanyaji wa mapato na inawapongeza sana kwa juhudi hizo na inandaa barua ya pongezi kulithibitisha hilo.

“Mwaka jana hadi robo ya pili inaisha halmashauri ya Mji ilikusanya milioni 200 sawa na asilimia 23 ya makisio ya bajeti ya mwaka 2017/2018 lakini kwa  kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 hadi robo ya pili inaisha halmashauri imekusanya zaidi ya shilingi 500 sawa na asilimia 67 kwa kweli mnastahili pongezi.” Alisisitiza Bwana Peter.

Aliongeza kwa kuwasihi viongozi wa halmashauri kuendelea kubuni mbinu zaidi za ukusanyaji wa mapato na kuongeza uwajibikaji na upendo ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mhe. Hamza Mafita alisema kuwa mapato yameongezeka baada ya Mkurugenzi kujipanga na timu yake na kuwezesha kufikia hapo na hiyo imetokana na kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya madiwani na menejimenti.

“Tumeongeza mashine za kukusanyia mapato hadi kufikia mashine 25 ambazo zimegawanywa katika kata mbalimbali kwa ajili ya kukusanya mapato na tuna mpango wa kufikisha mashine 50 ili kuhakikisha maeneo yote yenye mapato yanakusanywa.”Alisema Mhe. Hamza

Akielezea siri ya ukusanyaji wa mapato Mkurugenzi wa Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya watendaji na mikakati iliyowekwa katika ukusanyaji wa mapato.

“Tumeunda timu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato kwa kuweka mameneja ambapo kuna meneja wa POS, masoko na mageti ya mazao pamoja na hizo timu pia tumetenga siku maalum ya ukusanyaji wa mapato ambayo wakuu wa idara hujigawa na wasaidizi wao na kwenda kukusanya mapato.”Alisema Dakawa.

Hatahivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kutoa kodi kwani wakifanikisha hilo watawezesha halmashauri kujiendesha yenyewe lakini pia itasaidia serikali kupata mapato na kujiendesha yenyewe bila kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa