• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji yapongezwa ujenzi zahanati Chandimo kwa mapato ya ndani

Tarehe iliyowekwa: February 13th, 2025

Halmashauri ya Mji Kondoa imepongezwa kwa kusogeza huduma za afya kwa wananchi kwa kutoa mapato ya ndani zaidi ya shilingi milioni 70 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati katika Mtaa wa Chandimo. 

Pongezi hizo zimetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Thomas Rutachunzibwa mbele ya wananchi wa Chandimo Wakati wa ziara ya ufuatiliaji miradi ya maendeleo robo ya pili inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mji Kondoa.

Amesema ni Halmashauri imefanya jambo zuri sana hivyo wananchi wanapaswa kwa kuwaunga mkono katika kujitolea nguvu zao kwa kuwa Serikali hutoa fedha kwa maeneo yenye maboma lakini Halmashauri imejenga zahanati toka mwanzo yenyewe hivyo wanastahili pongezi.

Aidha amewataka wananchi wa mtaa wa Chandimo kujitolea kujenga wodi ya kujifungulia akinamama kwa kuwa jengo la zahanati ambalo lipo hatua za mwisho za ukamilishaji halina sehemu ya kinamama kujifungilia hivyo wahamasishane mmoja mmoja ili kuanza ujenzi huo.

“Nawapongeza sana kwa kujitoa kwenu kuja kufanya usafi katika zahanati yenu lakini nawashauri tu ili kuwasaidia akinamama zetu wajifungulie hapa tujitolee tujenge sehemu ya wao kujifungulia, shimo na kichomea taka na siyo kwamba jengo likikamilika hamtapata huduma hapana mtapata isipokuwa huduma ya kujifungua kwa akina mama,”amesema Dkt.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Serya Ndg. Hamisi Juma amemuhakikishia Mganga Mkuu kuwa watakwenda kutekeleza yote waliyoambiwa ambapo wataitisha mkutano wa Pamoja na wananchi ili kuwashirikisha ambapo baadhi ya wananchi waliokuwa eneo la Zahanati walikubaliana na ushauri uliotolewa.

Ameendelea kuipongeza Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya kata ya Suruke na ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Chemchem na kuwataka walimu kuyatunza madarasa hayo yatakapoanza kutumika.

Pia ameipongeza menejimenti kwa kuonyesha ushirikiano na uelewa wa miradi kwa Pamoja bila kujali kazi ya mtu hali inayoongeza uwajibikaji wa Pamoja jambo ambalo amesema hajaliona katika maeneo mengine.

Viongozi hao wametembelea miradi mbalimbali ikiwemo Zahanati ya Chandimo, Zahanati ya Ausia, vikundi viwili vinavyonufaika na mkopo wa asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri, mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Suruke na mradi wa ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Chemchem ambapo waliongozana na Kaimu Mkurugenzi Ndg. Irene Mosha na wataalam kutoka Idara na Vitengo.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa