• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji yatoa motisha kwa watumishi waliofanya vizuri ukusanyaji wa mapato 2024/2025

Tarehe iliyowekwa: July 8th, 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg.Said Majaliwa ametoa pongezi kwa watumishi waliofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Pongezi hizo zimeambatana na zawadi ya cheti pamoja na fedha taslimu Tsh 100,000 kama sehemu ya kuwashukuru kwa kufanya vizuri lakini pia kuwahamasisha watumishi wengine kufanya vizuri kwa kipindi kingine.

"Kwanza nawashukuru sana kwa namna tulivyosaidiana katika mwaka huu wa fedha, tumeandaa tuzo kwa watu ambao wamefanya vizuri"amesema Mkurugenzi Majaliwa

Hata hivyo Majaliwa amesema kuwa tuzo hizo zinatakiwa kuwa motisha kwa watumishi ambao hawajapata ili nao waweze kupata kwa msimu mwingine mwaka ulioanza wa 2025/2026.

Tuzo hizo zimetolewa kwa makundi ya Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Mitaa, Maafisa Ugani, Waganga Wafawidhi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati, pamoja na Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari.

Aidha katika kikao hicho imefanyika tathimini ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kuweka mikakati mbalimbali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato Ili kufikia lengo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo halmashauri inakusudia kukusanya bilioni 2.9.

"Humu ndani kuna Watendaji wa Kata na Mitaa, kila mmoja kwa nafasi  yake anawajibika kuhakikisha tunakusanya mapato ya Serikali"amesisitiza Mkurugenzi Majaliwa

Majaliwa ameeleza kuwa kila Mtendaji anapaswa kujua vyanzo vyake vyote vya mapato ili iwe rahisi kuvifuatilia kwa ukaribu pasipo kupoteza mapato ya aina yoyote.

Ameongeza kwa kuwaelekeza watumishi kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa mapato hususani ushuru wa mazao katika kipindi hiki cha mavuno lakini pia kutengeneza mfumo ambao mtu hawezi kuiba mapato ya halmashauri kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa mawakala.

Shughuli ya utoaji wa tuzo pamoja na kikao kazi imefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kondoa huku zaidi ya watumishi 60 wakihudhuria kikao hicho.

Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha Sita Kondoa Girls 2025 July 07, 2025
  • Tangazo la kazi za muda June 28, 2025
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji yatoa motisha kwa watumishi waliofanya vizuri ukusanyaji wa mapato 2024/2025

    July 08, 2025
  • Kondoa Mji yatoa milioni 90 ya Mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu awamu ya tatu

    July 01, 2025
  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa