• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji yawazawadia walimu waliofanya vizuri

Tarehe iliyowekwa: May 18th, 2021

Walimu wa Shule za Sekondari waliofanya vizuri katika masomo yao na shule zao Halmashauri  ya Mji Kondoa wametunukiwa vyeti na fedha taslimu ikiwa ni motisha kwao ili kuboresha ufundishaji na kuinua taaluma.

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa ambapo shule za Sekondari Bicha, Kondoa Islamic, Shule ya Wasichana Kondoa, Shule ya Sekondari Embeko  walimu wao wamezawadiwa kwa kufanya vizuri.

Akiongea  mgeni rasmi katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge ameeleza kuwa kwa sasa wameanza kupiga hatua katika upande wa elimu  na kueleza kuwa katika awamu hii mafanikio yatakuwa makubwa zaidi.

"Nawasihi sana viongozi wa elimu pamoja na walimu kuzidisha kupeana uzoefu katika masuala ya taaluma ili Halmashauri ya Mji Kondoa iweze kuongoza kimkoa katika sekta ya elimu,"amesema Mhe. Kiberenge.

Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Annette Nara ametoa takwimu za ufaulu kwa mwaka 2019 na 2020 ambapo ufaulu umeongezeka na ndiyo hali iliyowapelekea Idara kutoa zawadi kwa Halmashauri.

"Ili kujua kuwa shule za serikali za sekondari zinafanya vizuri au lah huwa tunazitenganisha na shule binafsi na  kwa kufanya hivyo tumefahamu kuwa mwaka 2020 ufaulu uliongezeka kutoka 71.77 hadi 76.81 na kufanikiwa kupunguza wanafunzi waliofeli kutoka asilimia 28.22 mwaka 2019 hadi 23.19 mwaka 2020,"amesema Afisa Elimu Sekondari Annette Nara

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Halmashauri ya Mji Kondoa diwani wa kata ya Chemchem Mhe. Zainabu Haroub amempongeza Afisa Elimu Sekondari kwa kuwashirikisha walimu wote na kuwapongeza walimu kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutawatia moyo walimu.

"Nashauri shule zinazofanya vizuri  kushirikiana na shule nyingine ili kuweza kuikuza sekta ya elimu Kondoa na naomba kamati za elimu zishirikishwe kuweza kuzungumza na wazazi kukuza elimu kwani hakuna ufaulu pasipo na mzazi,"amesisitiza Mhe. Zainabu

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu hao mara baada ya kupokeza zawadi wameeleza mbinu wanazozitumia katika ufundishaji zinachangia katika kukuza elimu huku pia wakizitaja changamoto kuwa ni wazazi kutokuwa na msukumo kwa watoto wao wanapokuwa shuleni.

Hafla ya kuwapongeza walimu wa Sekondari imefanyika ba kuwashirikisha Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara, Wakuu wa Shule aidha zawadi zilitolewa kwa shule zilizofanya vibaya ambazo ni Shule ya Sekondari Serya, Ula, Gubali na Dilai.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa