• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

LAAC yaishauri serikali kupeleka fedha Kituo Cha Afya Kolo

Tarehe iliyowekwa: March 16th, 2024

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali za Mitaa (LAAC) imeishauri serikali kupitia OR TAMISEMI kufanya tahmini na kupeleka fedha kwa ajili ya umaliziaji wa majengo ambayo hayajakamilika katika kituo cha Afya Kolo ili kitoe huduma iliyokusudiwa.

Ushauri umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Halima Mdee wakati akisoma taarifa ya majumuisho ya kamati katika mkoa wa Dodoma yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Kolo na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Wilaya ya Chamwino na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

“Tumeona kituo cha Afya Kolo kilipokea shilingi milioni 400 badala ya 500 zilizotengwa kwenye bajeti tunaishauri OR TAMISEMI kuwaleta milioni 100 iliyosalia kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la mama na mtoto likiwa limeunganishwa na jengo la upasuaji ili huduma stahiki ziweze kutolewa katika kituo hiki”amesema Mhe. Mdee

Aidha amewataka wataalam kutoka Halmashauri ya Mji Kondoa kufanya tathmini ya kazi iliyobakia ma kupata gharama halisi za fedha zinazohitajika kwa ajili ya kupeleka maombi hayo OR TAMISEMI kwa ajili ya kupatiwa fedha za kumalizia.

Ameongeza kuzitaja kazi ambazo hazijakamilika katika mradi huo kuwa ni pamoja na ujenzi wa kichomea taka, uwekaji wa marumaru na ufungaji wa bodi kwa jengo la mama na mtoto na upasuaji na kufanya marekebisho katika vibaraza kwa kufunga bodi ambazo hazijakaa sawa.

“Naomba muelewe kuwa kamati hii inashughulika na fedha za serikali za mitaa kwa kuzingatia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa fedha za serikali (CAG) baada ya kuona vitu ambavyo havijakaa sawa na tuliyoyaona tunatoa maelekezo ili yafanyiwe kazi ili tukirudi tena yasijitokeze tena,”amesisitiza Mhe. Mdee

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu OR TAMISEMI Ndg. Charles Msonde ameishukuru kamati kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwa inawasaidia kuongeza ufuatiliaji katika miradi na kuwaambia kuwa wameyapokea maelekezo yote ili miradi itekelezwe kwa manufaa ya wananchi na kuzitaka sekretarieti za mikoa kuongeza ufuatiliaji ili miradi itekelezwe kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Kolo Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho Ngd. Abubakari Mtundu ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuwajengea kituo hicho kwa kuwa kimekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Kolo kutokana na ajali zinazotokea katika Mlima wa Kwadinu ambapo majeruhi walikosa msaada wa haraka hivyo kupoteza maisha.

Kamati ya Bunge ya kudumu ya fedha za serikali za mitaa imefanya ziara katika halmashauri tatu za mkoa wa Dodoma ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Kondoa Mji na Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo ambapo katika Halmashauri ya Mji Kondoa imekagua Shule ya Sekondari Tura Day na Kituo cha Afya Kolo.

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Watumishi watakiwa kuendelea kutoa elimu ya stakabadhi ghalani

    June 23, 2025
  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa