• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Maafisa Elimu Idara ya Elimu Sekondari na Kata kurudi darasani kufundisha

Tarehe iliyowekwa: July 24th, 2019

Maafisa kutoka Idara ya Elimu Sekondari na Maafisa Elimu kata Halmashuari ya Mji Kondoa wamekubaliana kurudi darasani na kufundisha kwa kushirikiana na mwalimu wa somo husika ambapo watapanga utaratibu maalum ili kuhakikisha wanainua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne.

Azimio hilo limefikiwa leo katika kikao cha pamoja cha maafisa kutoka Idara ya Elimu Sekondari, Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule kilichofanyika katika kituo cha Walimu kilichopo Mtaa wa Iboni hivi karibuni.

Akiongea katika kikao hicho Kaimu Afisa Elimu Sekondari Pancracy Maleko alisema kuwa lengo la kuweka utaratibu huo ni kuhakikisha kuwa kila mtu kwa nafasi yake anakuwa anashiriki katika kuongeza ufaulu na kufuta daraja la sifuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu na bila kuathiri shughuli zao za kila siku.

“Sisi wote ni walimu tunaweza kufundisha ila si kwa kupangwa kwenye vipindi bali kwa kuweka utaratibu mzuri na walimu wa masomo husika na naamini hili linawezekana na litatuinua katika mtihani wetu wa mwisho.”Alisema mwalimu Maleko.

Aliendelea kueleza kuwa katika mtihani wa utahimilifu (Mock) mkoa halmashauri ya Mji Kondoa imeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza na kuwapongeza wakuu wa shule kwa kazi waliyofanya hadi kushika nafasi hiyo na kusema kuwa kwa mikakati iliyowekwa na Idara Halmashauri itaendelea kufanya vizuri ili kuendelea kushika nafasi ya kwanza kimkoa na kuendelea kufanya vizuri kitaifa.

Hata hivyo aliongeza kuwa Idara ina mpango wa kutengeneza mfumo ambao utakuwa na taarifa muhimu za shule zote ili kuachana na mazoea ya wakuu wa shule kuleta taarifa kila mara halmashauri ambapo kwa uwepo wa mfumo huo taarifa zote zitawekwa huko na kufanyiwa marekebisho kila mwezi hali ambayo pia itaokoa muda mwingi wa walimu wakuu.

Afisa Elimu Taaluma elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Alfred Jengo aliupongeza uongozi wa Shule ya Wasichana Kondoa kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka huu na kuwataka wazazi kufuata taratibu zilizowekwa kisheria katika kuwahamisha wanafunzi ili kuhakikisha mwanafunzi anakuwa salama.

Shule ya Sekondari ya Kondoa Islamic imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya na nafasi ya 12 kimkoa kati ya shule 251, Embeko imeshika nafasi ya pili kiwilaya na 18 kimkoa, Ibra imeshika nafasi ya tatu kiwilaya na 20 kimkoa na mwisho shule ya Sekondari ya Kolo ambayo imeingia katika shule 50 bora kimkoa.” Alisema Jengo

Katika kikao hicho wajumbe walipata nafasi ya kubadilishana uzoefu wa shule za serikali na binafsi na kuweka mikakati ya kuinua ufaulu wa shule za serikali ambapo walikubaliana walimu wakuu wote kuhakikisha walimu wanamaliza silabasi, kutoa mazoezi na majaribio ya kutosha, kutoa motisha kwa walimu watakaofaulisha vizuri na kugawa walimu kwa usawa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • "Sintamzibia ruhusa mtumishi anayetaka kwenda masomoni"- Mkurugenzi Majaliwa

    June 01, 2025
  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa