• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mafunzo MEK, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu yahitimishwa

Tarehe iliyowekwa: September 29th, 2021

Mafunzo ya uongozi kwa Maafisa Elimu Kata, Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Mji Kondoa kwa muda wa siku tatu yamehitimishwa rasmi na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kondoa.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa na kutolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha ADEM Bagamoyo ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kondoa Mwalimu Annette Nara amesema washiriki wote wanapaswa kudumisha ushirikiano na upendo miongoni mwao na wanaowaongoza katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.

"Nawasihi tusiombeane mabaya kwa kuwa wote ni viongozi na sisi siyo malaika na tusiache kuambiana mwenzetu anapokosea na mkimbiwa msishupaze shida ujirekebishe hakuna asiyekosea hata tukiambiwa na tunaowaongoza,"amesema Mwalimu Annette

Ameendelea kueleza kuwa wanapaswa kuheshimu nafasi zao kwa kuwa wanaowaongoza pia wana sifa za kuwa viongozi na wanatamani walipo hivyo ni bora wakashirikiana nao na kusaidiana nao katika kutimiza majukuju yao.

Kwa upande wake Mkufunzi kutoka Chuo cha ADEM Bagamoyo Venant Fundi amesema amefurahi kwa kuwa pamoja na viongozi hao na ana imani wamepata kitu kipya kutokana na mada zote alizowapatia na kuwashauri kumtumia vizuri Afisa Elimu  kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika kazi hiyo.

"Niwakumbushe kuwa nafasi zenu zinatamaniwa na watu wengi kwa kipindi tulichokaa hapa tumeondoa msongo wa mawazo na tumekuwa watu wamoja yaani Msingi na Sekondari msiende kujifungia mkashirikishane,"amesema Fundi

Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa mafunzo hayo Mwalimu Adam Awadhi amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya uongozi kwa Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule ambao wameteuliwa ikiwa ni pamoja na wa muda mrefu ili kuboresha utendaji kazi wao.

"Kiukweli mafunzo haya yamesaidia sana na kama yatatumiwa ipasavyo basi tutarajie makubwa na nimshukuru sana Mkurugenzi kwa kukubali mafunzo hayo kufanyika na walioratibu zoezi hilo kufanyika kwa kuwa hayajafanyika kwa kipindi kirefu,"amesema Mwalimu Awadhi

Mafunzo ya uongozi yamefanyika kwa siku tatu ambapo yamehudhuriwa na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule na Walimu wakuu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa viongozi hao na kuinua kiwango cha ufaulu.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa