• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Marufuku Kufanya Biashara Bila Kitambulisho Cha Ujasiriamali"- Dkt. Mahenge

Tarehe iliyowekwa: May 27th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amepiga marufuku wajasiriamali kufanya biashara  bila ya kuwa na  vitambulisho vya ujasiriamali katika masoko ya Wilaya ya Kondoa ikiwa ni pamoja na wakurugenzi kutowatoza ushuru wajasiriamali wenye vitambulisho.

Agizo hilo alilitoa katika kikao cha uhamisishaji  uuzaji wa vitambulisho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi Kondoa hivi karibuni.

“Mjasiriamali yoyote ambaye mauzo yake hayazidi shilingi milioni nne kwa mwaka lazima auziwe kitambulisho na akivae shingoni na naamini wapo wengi bado hawajauziwa hivyo tutoke kwenda kuwauzia na tuhakikishe kila mmoja ana kitambulisho.”Alisema Dkt. Mahenge.

Aliongeza kuwa halmashauri hazipaswi kuwatoza ushuru wajasriliamali wenye vitambulisho na kuwataka wajasiriamali wote ndani ya masoko kuweka utaratibu wa kuhakikisha soko linakuwa safi kutokana na takataka wanazozalisha sokoni hapo.

“Awali wajasiriamali wadogowadogo walikuwa wanazunguka na serikali ikaamua kuwarasimisha kwa kuanzisha vitambulisho ili watambulike  lakini hili pia limefanywa ili kuhakikisha kila mjasiriamali analipa kodi.”Alisisitiza Dkt. Mahenge.

Hata hivyo aliendelea kueleza kuwa kwa wajasiriamali kununua vitambulisho wanaongeza pato la serikali ambapo fedha zinazopatikana  zinasaidia katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege na ujenzi wa vituo vya afya nchi nzima.

Hata hivyo Dkt. Mahenge alitumia fursa hiyo kuwataka wakurugenzi kusimamia utekelezaji  agizo la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ambapo yatakoma ifikapo Mei 30, 2019.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa