• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mhe. Jafo aipa Kongole Halmashauri ya Mji Kondoa

Tarehe iliyowekwa: December 30th, 2020

Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo amewapongeza viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kusimamia vizuri miradi ya ujenzi wa madarasa na kuwataka kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa ya ukaguzi wa miradi na kuongea na watumishi akiongozana na wataalam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

“Kabla ya kuja hapa nilipita katika miradi nimekagua jengo jipya la Halmashauri jengo ni zuri hongereni linaendana na nyie ila lipo nyuma ya muda sijaridhika ikifika Februari 1 nataka Mkurugenzi na watumishi wako mhamie kule lakini miradi ya ujenzi wa madarasa ipo vizuri ila wakati mwingine mzingatie ushauri nilioutoa ili tuwe na majengo yatakayodumu kwa mufa mrefu,”amesema Mhe. Jafo

Aidha amewashauri kuongeza mapato kwa kubuni vyanzo vipya ambavyo havitawaumiza wananchi ili kupata fedha za kutosha kwa ajili ya kuiendesha Halmashauri na kuondokana na utegemezi wa serikali japokuwa wanafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.

“Watumishi wote fanyeni kazi kwa kujituma zaidi na mnapopewa kazi zifanyeni kwa wakati ila kubwa fanyeni kazi kwa kupendana kwani muda mwingi watumishi mnautumia mkiwa kazini katika baadhi ya maeneo watumishi wa idara moja hawaongei hii inapunguza pia utendajikazi kwani wanaopendana hufanyakazi vizuri,”amesisitiza Mhe. Jafo

Aidha amewataka Idara ya maendeleo ya Jamii kusimamia asilimia kumi za mapato na kuhakikisha zinawafikia walengwa kwani katika baadhi ya maeneo fedha hizo zimekuwa hazitolewi kutokana na wakurugenzi kuzuia fedha hizo kutoka na kuahidi kusimamia mapitio ya kanuni za mikopo hiyo ili sehemu ya marejesho zitumike kwaajili ya ufuatiliaji wa mikopo hiyo.

Hata hivyo amewaagiza Makatibu Tawala wa mikoa kufanya tathmini ya bei za dawa kwa mshitiri na bei ya soko ili dawa zipatikane vituoni na amemuagiza Mganga Mkuu kufunga mfumo wa kielektroniki katika vituo vya afya na zahanati ili kuzuia wizi wa dawa.

Akiongea awali Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Suleman Serea amemshukuru Mhe. Waziri kwa ziara yake ndani ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ambapo serikali imetoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi na kumuahidi kusimamia maagizo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha huduma inatolewa kwa wananchi.

Akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mkurugenzi Msoleni Dakawa amesema katika mwaka wa fedha 2017/18 halmashauri ilikisia kukusanya shilingi milioni mia 800 lakini mpaka kufika mwisho wa mwaka wa fedha ilikusanya shilingi bilioni 1.2 sawa na 133% na mwaka 2018/19 ilikisia kukusanya shilingi bilioni 1.6 mara mbili zaidi ya mwaka ulioisha na hadi kufikia 30 Juni 2019 Halmashauri ilikusanya shilingi 1.4 sawa na 88% hata hivyo kutokana na changamoto mbalimbali katika mwaka wa fedha 2020/21 imekisia kukusanya shilingi bilioni 1.4 na inaendelea kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kukusanya mapato mengi zaidi bila kumuathiri mwananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amemshukuru Mhe. Waziri kwa kuwatembelea na kumuahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na Mkurugenzi na watumishi wote ambao ana imani kubwa nao kutokana na utendaji wao mzuri kwa lengo la kuibadilisha Halmashauri ya Mji Kondoa.

Ziara ya Mhe. Jafo imefanyika ikiwa ni mwendelezo wake wa kutembelea Halmshauri na kukagua miradi ambapo alipata fursa ya kutembelea ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji Kondoa lililoghalimu zaidi ya shilingi bilioni 3, ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Maji ya Shamba na Shule ya Sekondari Ula ikiwa ni kati ya shule 7 zilizopokea shilingi milioni 291 na kuongea na watumishi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa