• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mhe. Rais, Ditopile watoa milioni 15 kwa Wanawake wa Vikoba Kondoa

Tarehe iliyowekwa: March 13th, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni kumi kwa wanawake wa vikoba katika Halmashauri ya Mji Kondoa na kuungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile kwa kuwachangia shilingi milioni tano.

Habari njema hizo zimetolewa na Mhe. Mariam Ditopile wakati akiongea katika kongamano la umoja wa vikoba katika Halmashauri ya Mji Kondoa akiwa mgeni rasmi lililoandaliwa na Shirika la msaada wa kisheria la JUST lililopo katika Halmashauri ya Mji Kondoa.

“Uongozi ni dhima kubwa na tumebeba maisha ya watu na tunafanya kila kitu kwa niaba yao hivyo viongozi tunapaswa kuzijua na kujali shida zenu japokuwa si rahisi kuzitatua zote ila tunapoweza tuwasaidie,”amesema Mhe. Ditopile

Ameongeza kwa kuwaambia wakinamama hao kuwa wafanye shughuli zao kwa amani kabisa kwa kuwa wapo kisheria na Katiba ya nchi inawatambua na serikali imeona umuhimu wa vikoba kwao ndio maana wamewatungia sheria ili kuwalinda hivyo amewapongeza JUST kwa kutoa elimu hiyo kwao.

“JUST mnafanya kazi kubwa sana hata kwa hili mnaunga mkono juhudi za Mhe. Rais anayewapambania wananchi wake usiku na mchana na hapa kuna madiwani wanawake hawa nao wanawapambania nyie kwenye vikao vya Halmashauri ili mpate fedha za asilimia kumi zitokanazo na makusanyo ya Halmashauri,”amesisitiza Mhe. Ditopile

Aidha amewataka kutokatishwa tamaa na wanasiasa wasioona umuhimu wa vikoba na kutoa kauli zisizofaa kwa kuwa wapo viongozi na wataalam wengi wamesomeshwa kwa kupitia vikoba na wananwake wengi kwasasa wamejiinua kiuchumi kwa kupitia vikoba na wasijidharau kwa kuwa vikoba ni utajiri.

“Naona pia mmempongeza Mhe. Rais kwa kufikisha miaka miwili madarakani kweli amefanya makubwa ikiwemo kujenga zahanati, vituo vya afya, ajira na kupandisha madaraja watumishi pamoja na kuwalipa kiinua mgongo waliotolewa kazini pamoja na hayo bado anaendelea kutafuta wadau wa maendeleo nje na ndani ya nchi tusiache kumuunga mkono na kutumia fursa zinazojitokeza kila wakati,”amesema Mhe. Ditopile

Akiongea awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amempongeza Mhe. Rais kwa kuleta fedha za utekelezaji wa miradi kwa wingi na kufungua fursa mbalimbali za nje na ndani ya nchi na kuwasihi wakinamama hao kutumia fursa za mikopo ya Halmashauri na kuipongeza divisheni ya Maendeleo ya Jamii kwa kusimamia vizuri zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia 10.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanavikoba waliofika Bi Salama amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwakumbuka wakinamama wa vikoba na kuwatungia sheria kwani awali walikuwa wanaona kama mchezo tu lakini kwasasa wanaishukuru Serikali kwa kuwakumbuka na wana imani watafanya makubwa zaidi.

 

“Tumeona mama akifanya makubwa ndani ya miaka miwili ambayo mengi yalisimama na tumeona fursa za wanawake na wasichana  kibao bila yeye yasingewezekana Mwenyezi Mungu azidi kumpa maisha marefu na tunamuahidi mwaka 2025 kura zaidi ya 2020 na fedha alizozipata tutazifikisha hadi kwa wenzetu wenye ulemavu,”amesema Bi. Salama

Kongamano la umoja wa vikoba Kondoa limefanyika kwa lengo la kutoa elimu ya masuala mbalimbali kwa wanavikundi wa vikoba ambapo mada za wosia,vikoba na usawa wa kijinsia zilitolewa ambapo vikundi vya vikoba vilihudhuria na mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mariam Ditopile ambaye alibeba kauli mbiu ya miaka miwili ya Mhe. Rais madarakani iliyosema “miwili ya mama hakuna kilichosimama, Kazi iendelee.

 

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa