• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mhe. Waitara awaasa wanafunzi Shule ya Wasichana Kondoa

Tarehe iliyowekwa: August 17th, 2020

Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara amewasihi wanafunzi wa Shule Sekondari ya Wasichana Kondoa kujifunga mikanda na kusoma kwa bidii ili wapate matokeo mazuri yatakayowawezesha kujiunga na vyuo vikuu watakavyo.

Ameyasema hayo alipokuwa anaongea na wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa baada ya kufanya ukaguzi wa majengo yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa ikiwa ni moja ya shule zilizopata fedha za ukarabati wa shule kongwe kutoka serikali kuu.

“Punguzeni usingizi wekeni ratiba ya kusoma ili mfaulu na nimepata taarifa zenu kuwa mnafanya vizuri nawapongeza bodi ya Shule, walimu na nyie wanafunzi kwa kuwa mnajisimamia vizuri na naamini kutoka hapa tutapata viongozi wazuri sana hapo baadae,”alisema Mhe. Mwita.

Aliongeza kuwa wanafunzi wametumwa elimu na si kubeba mimba kwa kuwa mtoto wa kike akisoma vizuri ana nafasi kubwa ya kuibadilisha familia na maisha yake kwa ujumla na muda wa wao kujipanga ni sasa ambapo wazazi wanawekeza kwao.

“Najua mmefurahia ukarabati uliofanyika kwa kuwa umeboresha mazingira ya  kujifunzia na kufundishia pongezi nyingi kwa Mhe. Rais wetu kwa kuona umuhimu wa kukarabati shule hii hivyo tumwombee aendelee kuwepo ili maono yake ya awamu ya pili yatimie,”alisisitiza Mhe. Waitara

Aidha aliwashauri viongozi wa Wilaya kushirikiana na wadau wengine ili kuboresha na kuisogeza mbele elimu kwa kuwa kuna mambo ambayo yanafanywa na serikali na mengine yanapaswa kufanywa na wadau ambao wanapatikana ndani na nje ya wilaya.

Aidha aliwapongeza viongozi kwa kusimamia vizuri fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ukarabati kwa kuwa kwenye baadhi ya maeneo yaliyofanya vibaya viongozi wameishia kwenye vyombo vya sheria na kuwasisitiza kusimamia majukumu yao yote vizuri na kuwashukuru walimu kwa kufanya kazi kwa kujitolea.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake Rais wa Shule ya Wasichana Kondoa Getrude Gadau amesema shule yao ina changamoto ya upungufu wa maji, ukosefu wa gari la shule kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za shule na ubovu wa barabara ya kufika shuleni hapo.

Akijibu changamoto hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa amesema kuwa changamoto ya barabara inaendelea kufanyiwa kazi kwa kuwa ipo katika miradi ya kimikakati na itawekewa lami na kuchimba kisima kirefu ambacho kitasaidia wanafunzi na wananchi wa jirani.

Mhe. Mwita Waitara ametembelea shuleni hapo na kukagua majengo yaliyokarabatiwa baada ya kupewa shilingi bilioni 1.12 katika mpango wa ukarabati wa shule kongwe na aliongozana na Mkurugenzi wa Elimu Msingi OR TAMISEMI.

  

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa