• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Milioni 27 za Mfuko wa Jimbo zagawanywa kuimarisha miradi

Tarehe iliyowekwa: March 17th, 2021

Kiasi cha shilingi milioni 27 kilichotolewa kwa ajili ya mfuko wa jimbo Halmashauri ya Mji Kondoa kimetolewa kwa ajili ya uimarishaji na ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi, sekondari na ofisi za mitaa.

Zoezi la ugawaji wa vifaa vya ukamilishaji wa miradi hiyo limefanyika katika ofisi za zamani za Halmashauri ya Mji likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mohamed Kiberenge akimuwakilisha mbunge wa jimbo la Kondoa Mjini Mhe. Juma Makoa.

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mhe. Kiberenge amewataka watendaji wa mitaa na waheshimiwa madiwani waliohudhuria katika makabidhiano hayo kwenda kuvitumia vifaa hivyo ipasavyo na kwa wakati ikiwemo saruji ili kuepusha kuganda na kupunguza ubora.

" Tumewakabidhi vifaa leo muende mkahamasishe wananchi wajitolee nguvu ili vitumike maana tunajua miradi ipo na inatekelezwa katika maeneo yenu tusijekusikia saruji imeganda kama awali" amesisitiza Mhe. Kiberenge.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa amewasisitiza watendaji kuvitunza vifaa hivyo kuvitumia ilivyokusudiwa na kuahidi kuchukua hatua za kiutumishi kwa wote ambao watasababisha uharibifu wa vifaa hivyo ikiwemo kulipa saruji kwa ambao zitaganda kwa uzembe.

Akisoma taarifa ya fedha za mfuko wa jimbo Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji kondoa Thecla Nyoni amesema kuwa fedha hizo zimeletwa kwa ajili ya kuchochea maendeleo katika miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Halmashauri.

"Mhe. Mwenyekiti fedha hizi milioni 27 zimegawanywa kwa kununua mifuko ya saruji 400, bati 62, nondo 35,tofali 200 na fedha taslimu shilingi milioni 17 zilizotolewa kwa ajili ya  utengenezaji wa madawati shilingi milioni 10, uezekaji wa madarasa Shule ya sekondari Bicha  shilingi milioni 5 na umaliziaji wa choo Shule ya Msingi Ubembeni shilingi milioni 2,"amesema Thecla

Zoezi la ugawaji wa vifaa limefanyika na kuhudhuriwa na Waheshimiwa madiwani wa kata ya Kilimani na Chemchem, Mkurugenzi wa Mji, watendaji wa mitaa, katibu wa mbunge na wataalam wa idara ya mipango na manunuzi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa