• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Miradi ya Wanufaika mikopo asilimia 10 Kondoa Mji yawavutia timu ya wakaguzi mkoa

Tarehe iliyowekwa: February 14th, 2025

Miradi inayotekelezwa na wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 iliyotolewa na Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kikundi cha vijana cha Mwangaza na kikundi cha mtu mwenye Ulemavu Hashim imewavutia timu ya mkoa iliyopita kukagua shughuli wanazofanya kutokana na ilivyowasaidia kuongeza kipato chao.

Akiongea kiongozi wa msafara huo ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Thomas Rutachinzibwa amesema amevutiwa na jinsi vikundi hivyo vinavyozalisha bidhaa ambazo zinaonekana na kuwataka wanufaika hao kuongeza bidi katika uzalishaji ili wakuze mitaji yao na kufanya vitu vikubwa zaidi.

“Kikundi cha Mwangaza ni vijana watupu mnaozalisha fenicha hongereni tuna Imani mnapata kazi nyingi sana kwasasa kama utengenezaji wa madawati na viti na meza kwa kuwa serikali inatoa fedha nyingi za utengenezaji wa fenicha hizo na hadi mlipofikia hapa naamini mtafika mbali zaidi,”amesema Dkt.

Aidha amempongeza Ndg. Kwa kuanzisha mradi wa mashine ya kusaga ambayo inafanya vizuri na inamwingizia kipato na kutaka awe mfano kwa watu wengine wenye ulemavu kwa kuwapa uzoefu wake ili waondokane na dhana za kuwa ukiwa mlemavu lazima uwe ombaomba.

“Kuna watu wengine ni wazima kabisa lakini hawajafanikiwa kufanya mambo makubwa kama haya nakupongeza sana na nashauri uombe mkopo mwingine ili uweze kufungua miradi mingine mingi zaidi ambayo itasaidia pia kuwamotisha wengine na ajira kutengeneza nafasi za ajira kwa wengine”amesisitiza Dkt.

Akiongea kwa upande wake Ndg. Hashim Hassan ameishukuru Halmashauri kwa kumuwezesha ambapo kwa mara ya kwanza walimuwezesha shilingi milioni tatu ambazo zilimsaidia kuanzisha mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa ambao unafanya vizuri hadi sasa kwa kumuingizia kipato cha kuendesha maisha yake.

“Nimeomba tena mkopo kwa Halmashauri ili uweze kunisaidia kununua gari la kusambaza unga nitakaozalisha ambapo kwasasa naona kama naibiwa ila nikiwa na gari nitaweza kupanda nami na kushiriki kwenye usambazaji, lakini kwasasa nimenunua mashine ya kufyatua matofali ya kisasa itakayoanza kazi muda si mrefu,”amesema Ndg.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Irene Mosha ameiambia kamati kuwa vikundi hivyo ni kati ya vinavyofanya vizuri kwa kuwa walishakopeshwa awali na wakarejesha bila changamoto zozote na wameomba tena na fedha zimeshawekwa benki.

“Huyu Hashim pia ni mtaalam anayetusaidia sana kwenye masuala ya mifumo kwa kuwaelekeza wanavikundi mbalimbali sababu hapa pia anatoa huduma ya mtandao na amesajiliwa kwenye mfumo wa manunuzi wa Nest Pamoja na kikundi cha Mwangaza ili wapate kazi za serikalini,”amesisitiza Ndg. Irene

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa