• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkurugenzi akutana na watendaji kuweka mikakati ya mapato 2024/2025

Tarehe iliyowekwa: July 16th, 2024

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amefanya kikao cha kimkakati  na Watendaji wa Kata na Mitaa kwa ajili ya kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yaliyowekwa ikiwa ni mwanzoni mwa mwaka mpya wa fedha 2024/2025. 

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji ambapo pia umehudhuriwa na Wakuu wa divisheni za Biashara, Kilimo na Mifugo, Utawala na Utumishi na vitengo vya Fedha, Mazingira, Huduma za Sheria na TEHAMA.

Akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi amewataka watendaji hao kuhakikisha wanakusanya mapato bila kuwabugudhi wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu tozo za serikali. 

Aidha amewataka watendaji hao kuelewa majukumu yao katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku katika maeneo yao na kuhakikisha kila siku wanakusanya ushuru au kila wiki ili kufikia malengo yaliyowekwa kwenye bajeti ya 2024/2025.

"Nawaomba sana mzitunze na kuzilinda mashine za kukusanyia mapato hizo ni kama silaha lakini pia mjue idadi yake katika maeneo yenu kwa namba na kuzikagua kila siku ili tusiwe na mashine feki katika maeneo yetu msipofanya hivi ntajua nyie pia ni sehemu ya ubadhilifu utakaofanyika" amesema Mkurugenzi Majaliwa. 

Ameendelea kuwasisitiza kutoa taarifa za changamoto watakazokutana nazo wakati wa kukusanya mapato ili zipatiwe ufumbuzi na kuahidi kutoa motisha kwa watendaji watakaofanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato kila mwezi. 

Hata hivyo amewasihi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utaofanyika mapema mwaka huu.

Kwa upande wao wakuu wa divisheni na vitengo waliohudhuria kikao hicho wamesisitiza suala la ukusanyaji wa mapato katika nyanja zote ikiwemo kukusanya fedha za taka ili zisaidie kuuweka mji katika hali ya usafi.

Matangazo

  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Kondoa Mji watoa mafunzo kwa vikundi 16 vya mikopo awamu ya tatu

    June 24, 2025
  • Wataalam wa Kilimo na Mifugo Kondoa Mji watembelea Nanenane Jijini Dodoma

    June 24, 2025
  • Watumishi watakiwa kuendelea kutoa elimu ya stakabadhi ghalani

    June 23, 2025
  • Baraza Maalum Kondoa Mji lapitisha Sheria ndogo kuimarisha vyanzo vya mapato

    June 20, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa