• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkurugenzi apongezwa kwa ujenzi wa zahanati kwa mapato ya ndani

Tarehe iliyowekwa: February 27th, 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amepongezwa na Dkt. Rashid Mfaume ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na ustawi wa jamii kutoka OR- TAMISEMI kwa kutenga fedha za mapato ya ndani shilingi milioni  77,626,869 na kujenga Zahanati ya Ausia ili kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.

Dkt. Mfaume ametoa pongezi hizo alipotembelea Zahanati ya Ausia iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa na kusema kuwa wamezunguka halmashauri nyingi zenye mapato makubwa lakini bado wameshindwa kutenga mapato ya ndani na kujenga Zahanati.

" Halmashauri ya Mji Kondoa ina mapato kidogo sana, hata bilioni 2.5 hayafiki lakini Mkurugenzi amefanikiwa kutenga mapato ya ndani na kujenga Zahanati, kwa kweli nampongeza sana" amesema Dkt.Mfaume

Dkt.Mfaume akiwa na wataalamu wenzake kutoka OR -TAMISEMI akiwemo Mganga Mkuu wa mkoa wameanza ziara ya kukagua huduma za afya, lishe, na ustawi wa jamii katika Halmashauri za mkoa wa Dodoma.

Pia Mkurugenzi huyo amewasihi wasimamizi na watumishi kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa sekta ya afya ili kuwezesha wananchi kupata huduma iliyo bora zaidi.

"Serikali imekuwa ikitafuta fedha mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya ili kuboresha huduma kwa wananchi, hivyo ni muhimu kwa wasimamizi na watendaji kuzingatia ubora na ufanisi katika utekelezaji wa miradi hiyo" amesisitiza Dkt.Mfaume

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg.Said Majaliwa ameshukuru kwa ujio wa ugeni huo na kuahidi kufanyia kazi baadhi ya changamoto ambazo zimeibuliwa na wataalam hao.

Dkt. Mfaume na wataalamu wenzake wamefanikiwa kutembelea  kituo cha Afya Kingale, Zahanati ya Ausia, Kituo Cha Afya Serya pamoja na Hospitali ya Mji Kondoa ambapo wametoa maelekezo ya kutatua changamoto zilizopo ili kutoa huduma zilizo bora lakini pia wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi wa Hospitali ya Mji Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa