• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkurugenzi Kondoa Mji afanya hafla kuwaombea wanafunzi darasa la saba 2025

Tarehe iliyowekwa: September 4th, 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg.Said Majaliwa ameandaa hafla ya chakula cha pamoja kwa wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajiwa kufanya Mitihani yao ya Taifa tarehe 10 na 11 mwezi wa 9, mwaka 2025.

Tukio hilo la chakula cha pamoja limeambatana na maombi maalumu kwa ajili ya kuwaombea wanafunzi hao ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanya mtihani wao wa Taifa.

Hafla hiyo imefanyika katika shule zote 35 za msingi zenye wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka 2025.

Akiongea, katika shule ya msingi Ubembeni ambapo alikuwa mgeni rasmi,  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg.Said Majaliwa  amesema Halmashauri imetenga siku ya tarehe 4 mwezi Septemba, mwaka 2025 kuwa ni ya  wazazi, walimu, wanafunzi, kamati za shule, viongozi wa mtaa na kata pamoja na viongozi wa dini kula chakula cha pamoja na kuwaombea wanafunzi wa darasa la saba ambao wiki lijalo watafanya mtihani wa Taifa.

Jumla ya wanafunzi 1881 wakiwemo wavulana 908 na wasichana 973 wa darasa la saba wa mwaka 2025 katika Halmashauri ya Mji Kondoa, wanategemewa kufanya mtihani wao wa Taifa.

Akiongea na wanafunzi hao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa  amemshukuru Afisa Elimu Msingi Bi Lucy Mbolu kwa maandalizi ya  tukio hilo muhimu.

 Aidha, Mkurugenzi amewashukuru wazazi kwa kufika shuleni hapo na kujumuika na watoto wao kupata chakula Cha pamoja.

"Niwashukuru sana wazazi wenzangu, Urithi pekee unaodumu kwa mtoto ni elimu pekee" Said Majaliwa.

Kabla ya kuanza kupata chakula hicho wanafunzi hao wameombewa na viongozi wa madhehebu  mbalimbali ya dini Ili kuweza kufanya vizuri katika mtihani wao wa Taifa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini pamoja na viongozi wa serikali.

Majaliwa amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea  kumuomba mwenyezi Mungu Ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao.

"Sisi kama Halmashauri tutahakikisha tunazingatia suala la salama wenu ili muweze kufanya mtihani wenu kwa amani na utulivu" Majaliwa.

Majaliwa pia ametumia fursa hiyo kuwaambia wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura pindi tarehe ya Uchaguzi itakapowadia mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka, 2025.

Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha Sita Kondoa Girls 2025 July 07, 2025
  • Tangazo la kazi za muda June 28, 2025
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili Kondoa Mji June 13, 2025
  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • DC Nyangasa aongoza kikao cha tathmini ya lishe Kondoa Mji

    September 10, 2025
  • Kondoa Mji wafanya ziara ya kujifunza Dodoma Jiji

    September 05, 2025
  • Mkurugenzi Kondoa Mji afanya hafla kuwaombea wanafunzi darasa la saba 2025

    September 04, 2025
  • RC Senyamule ahitimisha wiki ya Elimu ya Watu Wazima

    August 18, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa