• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Mpeni ushirikiano Mkurugenzi Majaliwa" - Mkurugenzi Sweya

Tarehe iliyowekwa: March 17th, 2024

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndg. Paul Sweya amewashauri Wakuu wa Divisheni na Vitengo katika Halmashauri ya Mji Kondoa kumpa ushirikiano Mkurugenzi Said Majaliwa aliyehamishiwa katika Halmashauri hiyo ili kurahisisha utendaji kazi wake.

Ushauri huo ameutoa wakati wa makabidhiano ya ofisi kati ya wakurugenzi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge, Makamu Mwenyekiti Mhe. Zainabu Haroub na Wakuu wa Divisheni na Vitengo.

“Kipo kibaya nilichowafanyia na kipo kizuri nilichowafanyia mi si malaika msiniwekee doa nikaenda na kinyongo mnisamehe kwa dini zenu wakristo na waislam nami nitawaombea huko ninakokwenda Mkurugenzi nakukabidhi watumishi wote wapo vizuri ila muda utaongea,”amesema Mkurugenzi Sweya

Aidha amewaomba wakuu wa divisheni na vitengo kutomuharibu Mkurugenzi na kuwaomba kumsaidia kwa kufanya kazi kwa ushirikiano naye kwa kuwa ana safari ndefu katika uongozi na baadhi ya watumishi hawana tabia ya kuwasaidia wenzao.

Akifungua kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Zainabu Haroub amewataka Wakuu wa Divisheni na Vitengo kwa nafasi walizonazo kumueleza Mkurugenzi changamoto wanazokabiliana nazo ili kuzitatua pamoja na kusonga mbele.

“Mkurugenzi tunayo miradi mingi ipo ambayo imefanyika na ipo ambayo inaendelea kufanyika lakini nina imani viongozi hawa watakupa ushirikiano utaifahamu miradi yote na changamoto zilizopo katika miradi,”amesema Mhe. Zainabu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Mohamed Kiberenge amesema kama Waheshimiwa Madiwani kwa kipindi chote wameishi na Mkurugenzi Sweya vizuri kwa kuwa aliweza kusimamia stahiki zao na kuhakikisha wanazipata kwa wakati na aliwamotisha kama watumishi wengine ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza na kuwaheshimu.

“Mkurugenzi hawa ni watumishi wetu hakuna mbaya wote unaweza ukawafanya wakawa daraja la kwanza inawezekana wakaweza kushindana mbio tu ukawapanga katika madaraja na nawasihi watumishi fanyieni kazi suala la mapato sababu ndio kila kitu katika Halmashauri,”amesisitiza Mhe. Kiberenge

Mkabidhiano ya ofisi yamefanyika baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwateua viongozi wapya na wengine kuwahamisha ambapo Halmashauri ya Mji Kondoa ameletwa Mkurugenzi Ndg. Said Majaliwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga na aliyekuwa Mkurugenzi Ndg. Paul Sweya kuhamishiwa katika Halmashauri ya Mbeya.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa