• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mwenge wa Uhuru wapitia miradi ya Bilioni 1.5 Kondoa Mji

Tarehe iliyowekwa: July 30th, 2024


Mwenge wa uhuru umekimbizwa katika Halmashauri ya Mji Kondoa na kupita katika miradi 6 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.

Miradi iliyopotiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa vijana Wazalendo uliopo Kwantis, Zahanati ya Choka, usambazaji maji Hachwi, barabara Gubali Bolisa- Iboni, Bweni la watoto wenye mahitaji maalum Iboni na mradi wa msitu wa miombo Hachwi.

Akiongea katika mradi wa Hachwi kiongozi mkimbiza Mwnge Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava amewahakikishia wananchi wa Hachwi kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati na kutoa huduma kusudiwa kwa jamii ambapo kwasasa upo asilimia 90 ya utekelezaji na una thamani ya shilingi milioni 800 na unatarajia kuwanufaisha wananchi zaidi ya 2000.

Aidha katika mradi wa zahanati ya Choka kiongozi mkimbiza Mwenge ametaka zahanati hiyo kukamilishwa kwa wakati ili wananchi wa Mtaa wa Choka na mene jirani wapate huduma ya afya katika kituo hicho kama ilivyokusudiwa na serikali, ambapo mradi huo umegharimu shilingi 87.3 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu na mapato ya ndani.

Katika mradi wa vijana Mkimbiza Mwenge kitaifa amewataka vijana kutumia fursa za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ili kujikomboa kiuchumi na kujipaia kipato kwa kuwa mikopo hiyo haina riba na kuwapongea kikundi hicho kwa kumaliza mkopo wa shilingi milioni 8 kwa wakati huku wakifungua maduka mawili inayowasaidia kujipatia kipato.

Katika hatua nyingine akiwa katika mradi wa misitu wa miombo amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira na kutahifadhi na kufanya kilimo ambacho kitakuwa endelevu kwa utunzaji na uhifadhi wa mazingira na kuachana na tabia ya kufuga mifugo kwa kuzurulisha nakuharibu mazingira.

Akiongea na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika mradi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum amewahakikishia wanafunzi hao kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo pamoja nao na ndio maana anaendelea kuleta fedha za koboresha mazingira yao ya kujifunzia ambapo bweni hilo limegharimu shilingi milioni 142.9 kutoka TEA.

Kwa upande wake Mbunge wa Kondoa Mjini Mhe. Ally Makoa amemshukuru Rais kwa kuleta fedha zote ndani ya jimbo la Kondoa Mjini ambazo zimewasaidia wananchi kutatua changamoto za muda mrefu ikiwemo mradi wa maji Hachwi ambako kwa mara ya kwanza wanaenda kupata maji ya bomba.

Mwenge wa Uhuru umepitia miradi yote hiyo na kuweka mawe ya msingi, kufungua na kuona ambapo viongozi mbalimbali wameshiriki ikiwemo waheshimiwa wabunge, viongozi wa Chama na wananchi ambapo mkesha wake ulifanyika katika uwanja wa Sabasaba tarehe 30.06.2024 na kukabidhiwa Halmashauri ya Wilaya tarehe 1.07.2024.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa