• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mwenge wachangia ujenzi zahanati gereza la Kondoa

Tarehe iliyowekwa: July 27th, 2021

Mwenge wa Uhuru umeunga mkono juhudi za ujenzi wa Zahanati Gereza la Kondoa Mjini kwa kuchangia shilingi laki tatu na kuendesha harambee fupi kwa viongozi iliyopelekea kukusanya shilingi milioni 2.8.

Zoezi hilo limeongozwa na Mkimbiza Mwenge kitaifa LT. Josephine Paul Mwambashi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Gereza la Kondoa Mjini wakati wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Kondoa hivi karibuni.

"Nichukue nafasi hii kuwapongeza viongozi na watumishi wa gereza la Kondoa kwa kuamua kufanya jambo hili la kujenga zahanati kwani pamoja na kuwasaidia wao tu itaboresha afya za wananchi wote wa Kondoa,"amesema LT. Josephine

Aidha amesema anajua mradi huo unaenda taratibu kwa kuwa hawana chanzo cha uhakika cha fedha za ujenzi zaidi ya kutafuta kutoka maeneo mbalimbali ndio maana ameona ni vyema kupitia mbio hizo wakachangia kiasi cha fedha ili kumalizia mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amewashukuru wakimbiza Mwenge kitaifa kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo za umaliziaji na kuweka jiwe la msingi na kwa upande wake atahakikisha anausimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kutoa huduma.

Akisoma taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkuu wa Gereza Afande Kurwa Nasibu Mwakasikwa amesema mradi huo hadi kufikia hatua hiyo wametumia shilingi milioni 31 fedha zilizotokana na mapato ya zahanati ya sasa, nguvu za wananchi na wadau wa maendeleo.

Mwenge wa Uhuru umekimbizwa Wilaya ya Kondoa tarehe 27.7.2021 ambapo umezindua miradi mitatu na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili yenye jumla ya shilingi 893,238,921.30 na kwa mwaka huu kauli mbiu inasema" TEHAMA ni msingi wa taifa endelevu, itumie kwa usahihi na uwajibikaji".

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa