• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Ushirikiano wasisitizwa ujenzi wa madarasa ya pochi la mama

Tarehe iliyowekwa: October 5th, 2022

Ushirikiano kati ya Wakuu wa Shule na Ofisi ya Mkurugenzi umesisitizwa wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa madarasa 9 yenye thamani ya shilingi milioni 180 fedha kutoka serikali kuu maarufu kama pochi la mama.

Msisitizo huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Sweya kwa Wakuu wa Shule wakati wa kikao cha kujadili namna ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa hayo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji.

“Changamoto zikitokea mtoe taarifa mapema msisubiri hadi sisi tuje huko kama viongozi ndio tuwalalamikie nyie tutawavunja moyo kwanza lakini pia tutatengeneza gap la uhusiano mi nakuja na kuanza kufoka unajisikiaje wewe wakati kumbe umefanya kazi kubwa ila  tu sikuwa na taarifa,”amesema Mkurugenzi Sweya

Aidha amesema mwisho wa utekelezaji wa mradi huo ni Desemba 15 ikiwa ni maagizo ya Mhe. Rais na yeye yupo kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya viongozi na hatakuwa Mkurugenzi wa maelezo bali Mkurugenzi Mtendaji wakati wote wa utekelezaji wa mradi huo.

“Mmetekeleza miradi hapa karibuni naamini mtatumia uzoefu wa miradi ya nyuma penye mapungufu mliona na nasisitiza thamani ya fedha ionekane na vifaa vikaagizwe kwa mujibu BOQ na mradi uishe na mradi huu si wenu peke yenu tutakuwa pamoja na sisi tunawaamini na kuwaheshimu na utaalam wenu,”amesisitiza Mkurugenzi Sweya

Hata hivyo amewataka Wakuu wa Shule kuepuka kuongeza bei ya vifaa na kujiingiza katika kupata fedha kutoka kwa wazabuni kwa kuwa fedha hizo zitafuatiliwa na kuagiza vifaa kununuliwa kwa pamoja ili kuokoa fedha na muda.

Akiongea katika kikao hicho Kaimu Mweka Hazina Ndg. Rahabu Sanga amewataka Wakuu wa Shule kuandaa mapema nyaraka zote za mradi wakati wa kuomba malipo na kuwasimamia mafundi watakaopata kazi ili wafungue akaunti na malipo yao yaingie kwenye akaunti zao moja kwa moja na si walimu kwenda kuwalipa.

Kaimu Mhandisi Ujenzi Mhandisi Jeremiah Longido amewataka Wkuu wa Shule kuajiri mafundi wenye uwezo na wanaofuata maelekezo wanayopewa na kuongeza  kuwa kwa mujibu wa mpangokazi uliotolewa na ofisi ya Mkurugenzi madarasa yatakamilika ifikapo Desemba mosi,2022.

Akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Shule Mwalimu Zakayo Simanjiro amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia fedha hizo za ujenzi wa madarasa na kuahidi kwenda kutekeleza mradi wa madarasa kwa viwango vinavyotakiwa.

Halmashauri ya Mji Kondoa imepata fedha shilingi milioni 180 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 9 na yatajengwa katika Shule za sekondari za Ula, Bicha, Gubali, Kwapakacha na Dilai.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa