• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Pendekezo Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 kuwanufaisha wafugaji Dodoma

Tarehe iliyowekwa: February 5th, 2020

Kamati ya Siasa Mkoa wa Dodoma imeliweka suala la kuongeza thamani mazao ya mifugo katika Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 kutokana na kuongezeka kwa ufugaji mkoani humo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Mhe. Godwin Mkanwa wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa katika Wilaya ya Kondoa.

“Tunapenda Dodoma kiwanda kikubwa cha nyama kijengwe, kiwanda kikubwa cha ngozi kijengwe ili ngozi zote zinazotokana na machinjio hizi basi ziweze kupata soko lake kwa kuwa na sisi ni wafugaji wakubwa katika mkoa,”alisema Mhe. Mkanwa.

Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda kikubwa cha nyama kutasaidia kuiongezea thamani kwa kuifungasha vizuri na kupata soko la uhakika jambo ambalo litawafanya wafugaji wapate maendeleo na kujiinua kiuchumi.

Aidha alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota kwa usimamizi mzuri wa miradi ndani ya wilaya ya Kondoa na kusema kuwa katika mradi wa machinjio katika mnada wa Bicha walioutembelea Kondoa Mji thamani ya fedha iliyotumika inaonekana na inaridhisha.

Awali akisoma taarifa ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika mnada wa Bicha Kaimu Afisa Mifugo Dennis Moshi alisema kuwa mradi huo umejengwa na wadau wa maendeleo shirika la LIC ambao walitoa shilingi milioni 51 na Halmashauri kuchangia shilingi milioni 2.

“Mradi huu umelenga katika kuboresha mazingira ya kibiashara ya mifugo, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha ulinzi wa mifugo ya wafanyabiashara wa mifugo katika mnada ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma kwa jamii inayozunguka kata za Halmashauri ya Mji na wilaya za jirani za Kondoa na Chemba,”alisisitiza Bwana Dennis.

Kamati ya siasa mkoa wa Dodoma ipo katika ziara ya kutembelea miradi ndani ya mkoa wa Dodoma na iliambatana na baadhi wajumbe wa kamati kuu toka taifa na mkoani ikiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • "Sintamzibia ruhusa mtumishi anayetaka kwenda masomoni"- Mkurugenzi Majaliwa

    June 01, 2025
  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa