• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Prof. Ndalichako awafunda wanachuo cha Bustani Kondoa

Tarehe iliyowekwa: June 17th, 2020

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanachuo wa Chuo Cha Ualimu Bustani Wilaya ya Kondoa kuwa wazalendo kwa kuipenda na kuitetea nchi ya Tanzania ili iweze kufikia uchumi wa kati.

Ujumbe huo ameutoa wakati akiongea na wanachuo wa Chuo hicho alipofanya ziara ya kutembelea chuoni hapo hivi karibuni kujionea utendaji wa kazi wake na ukarabati wa chuo unaoendelea chuoni hapo.

“Jana tumemsikiliza Mhe. Rais wakati akisoma utekelezaji wa serikali ya awamu ya tano kwa upande wa elimu makubwa yamefanyika nyie mmekuwa mashuhuda ikiwemo elimu bure ambapo kila mwezi zaidi ya shilingi bilioni 24 hutolewa, uboreshaji wa miundombinu ya madarasa na mabweni katika vyuo na shule kongwe hata hapa shuleni mmeona ukarabati unaoendelea ambapo zaidi ya shilingi milioni 874 zimeletwa,”alisema Prof. Ndalichako.

Aidha amewakumbusha kuwa uzalendo ni pamoja na kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali ikiwemo ujenzi wa madaraja, umeme wa REA, ujenzi wa vituo vya afya pamoja na ujenzi wa barabara za lami na kuwataka kuacha kurubuniwa na wanaoisema vibaya serikali.

“Tunaelekea kwenye uchaguzi Mkuu kuweni makini msikubali kutumiwa vibaya na watu wasiyoitakia mema nchi mkae na kuthamini mambo na siku zote wanasema akili za kuambiwa changanya na za kwako tutunze amani, umoja na mshikamano uliopo ambao uliasisiwa na viongozi wetu waliotangulia mbele za haki,”alisisitiza Prof. Ndalichako.

Hata hivyo aliwasihi kutoichezea amani iliyopo kwa kuwa nchi zingine wanahangaika kuirejesha amani ambayo walichezea na wanapata shida hadi leo kwani ni rahisi kuivunja amani ila ni gharama sana kuirejesha amani kama ilivyokuwa awali na nchi ya uchumi wa kati itafikiwa iwapo kila mtu atatimiza wajibu wake.

Kwa upande wao wawakilishi wa wanachuo waliishukuru serikali kwa kupunguza ada ya chuo kutoka shilingi laki sita hadi kufikia shilingi laki nne na nusu na kuiomba serikali kuwapatia ajira kwa wakati muafaka mara wanapomaliza chuo ili kuepuka kupoteza maarifa waliyoyapata chuoni na kuboresha mtaala wa elimu ya awali.

Ziara ya Profesa Ndalichako ameongozana na wakurugenzi mbalimbali wa Wizara ya Elimu ambapo alipata fursa ya kusikiliza taarifa ya Chuo, kukagua ukarabati wa chuo unaofanyika ikiwa ni moja ya vyuo 25 vilivyokarabatiwa na serikali ya awamu ya tano na kuongea na wanachuo 556 ambapo pia Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota na wataalam mbalimbali walishiriki katika ziara hiyo.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa