• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Rais amaliza mgogoro wa wananchi na Gereza la King'ang'a

Tarehe iliyowekwa: February 5th, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemaliza mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wananchi wa kata ya Kingale na gereza la King’ang’a uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 kwa kugawa eneo lililokuwa linagombaniwa nusu kwa nusu.

Tamko la kumaliza mgogoro huo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Masauni Masauni wakati wa mkutano na wananchi wa Kata ya Kingale uliofanyika katika kata hiyo hivi karibuni.

“Leo hii tumekuja na habari njema kwa wana Kingale kuwa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa kutoa suluhu ya matatizo yaliyoshindikana na kukomaa ametoa suluhu kwa wananchi wa Kingale, ukiacha historia ya ukubwa wa eneolililokuwa lina mgogoro kati ya magereza na wananchi wa Kingale ambalo lilikuwa na ukubwa wa ekari 7495.74 Mhe. Rais ameelekeza ekari 3272.4 libaki kwa wananchi na kuendelea kulitumia kwa shughuli za kilimo na mifugo na shughuli zingine za kiuchumi,”amesema Mhe. Senyamule

Aidha ameongeza kuwa ekari zinazibaki zibaki kwa ajili ya matumizi ya magereza kwa shughuli zao zote ambalo ni karibu ya nusu ya eneo na hii imedhihirisha kuwa Mhe.Rais yupo kwa ajili ya wananchi kwa kuwa angeweza kusema kwasababu eneo hilo limekuwa linatumiwa na Magereza kwa kipindi kirefu basi lingebaki kwa Magereza.

“Eneo hili baada ya kutolewa inatakiwa kufanyika mambo yafuatayo kwanza watu wa ardhi ndani ya mwezi mmoja waje wafanye utaratibu wa kuonyesha mipaka halisi ya maeneo yalivyogawanywa kwa kushirikiana na magereza wenyewe pamoja na viongozi wa vijiji eneo lipimwe na liwekwe mipaka halisi na ziwe kubwa na zionekane na kila mmoja,”amesisitiza Mhe. Senyamule

Ameendelea kuwaagiza viongozi wa maeneo hayo kuendelea kutunza mipaka ili kuzuia muingiliano ikiwa ni pamoja na magereza ikiwa ni pamoja na kuwashauri Wizara ya Kilimo kuweka utaratibu wa kuweka bwawa kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji kwa kuwa eneo hilo ni bonde na Wizara ya Mifugo kujenga majosho na mabwawa kwa ajili ya kunyweshea mifugo ya wananchi wa kata ya Kingale.

Akiongea wakati wa mkutano Mbunge wa Kondoa Mjini Mhe. Ally Makoa amesema mapendekezo yaliyotoka kwa wananchi ya kilometa 1.5 waachiwe magereza na kilometa 1.5 Kambi ya Moto hadi kwenye mbuyu hivyo wao wataendelea na eneo lao la kilometa ambalo hajawalima ambalo kwa sasa ni wazi na walipokuwa wakiingiza mifugo yao walikuwa wanakamatwa.

“Shukrani kubwa kwa Mhe. Rais na Wizara ni kutuleta wataalam kutoka Wizara ya kilimo kwa ajili ya kutuwekea miundombinu ya umwagiliaji katika eneo lile ili tunyweshwe mifugo yetu na tulime tumwagilie wakati wote na mkumbuke hii hi Halmashauri ya Mji kuna wakati Mkurugenzi atazuia kulima na ndio maana tunaweka kulimo cha mjini,”amesisitiza Mhe. Makoa

Mwakilishi wa wananchi wa Kingale amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia eneo lililokuwa linangojewa kwa muda mrefu na kumuomba Mkuu wa Mkoa watu wa ardhi kwenda haraka kwa kuwa wapo na wazingatie maagizo ya Mhe. Rais kuhusu mipaka.

Mgogoro wa ardhi kayi ya wananchi wa kaya ya Kingale na gereza la King’ang’a umedumu kwa zaidi ya miaka 30 ambapo eneo lililokuwa linagombaniwa lilikuwa na ukubwa wa ekari 7495.74.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa