• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Programu ya Shule Bora itasaidia kuinua kiwango cha ufaulu Dodoma"- Dkt. Fatuma

Tarehe iliyowekwa: January 27th, 2023
KATIBU tawala Mkoa wa Dodoma Dk.Fatuma Mganga amesema kuwa moja ya matamanio yaliyopo kwa sasa mkoani hapo kwa mwaka 2023 ni kuongeza ufaulu kwa asili 95 ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba na angalau asilimia 75 ya wanafunzi wanaohitimu kidato Cha Nne Wawe na ufaulu wa daraja la 1-3.

Dkt.Mganga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya program ya Serikali ya SHULE BORA kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika Januari 27,2023 wilayani Kondoa.

Mradi wa Shule Bora ni Programu ya Serikali Tanzania,ikifadhiliwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la kuinua ubora wa elimu ya Awali na Msingi katika mikoa tisa (9) hapa nchini kwa ushauri elekezi kutoka Cambridge Education ikishirikiana na mashirika ya ADD International, International Rescue Committee na Plan International.

"Mradi huu wa Shule Bora unatupa nguvu na matumaini makubwa kama mkoa kuona kuwa tunaweza kufikia malengo yetu angalu kuongeza ufaulu kwa asili 95 ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba na angalau asilimia 75 ya wanafunzi wanaohitimu kidato Cha Nne Wawe na ufaulu wa daraja la 1-3,"amesema Dk.Mganga

Hata hivyo Katibu tawala huyo amesema kuwa swala la Elimu katika Mkoa wa Dodoma bado halijatangazwa vizuri na kuwataka waandishi wa habari wakawe chachu katika kuielimisha jamii kuwa wanajukumu la kushiriki kikamilifu katika kuboresha elimu.

"Naamini mara baada ya kumalizika kwa mafunzo haya mtakwenda kuifungua jamii kifikra kuwa wana jukumu la kushiriki katika kuinua ubora wa elimu katika Mkoa wetu na naomba sana kwenu waandishi mwaka huu Dodoma tumebeba agenda yetu ya sekta ya elimu hivyo kupitia nyinyi tunaamini itafanikiwa kwani nyinyi mkiamua kutumia vyombo vyenu vizuri hakuna kitakachoshindikana,"ameongeza Dkt.Mganga

Ambapo Dkt.Mganga ameeleza kuwa kwa sasa mkoa wa Dodoma una upungufu wa vyumba vya Madarasa zaidi ya 7000 ndipo akapeleka ombi kwa wazazi na jamii kwa ujumla kujikita katika kuhakikisha kila mwaka katika gitongoji,kata na mitaa yao wanaweza kujenga angalau chumba kimoja cha darasa ili kuwasaidia watoto wenye umri wa kwenda shule kuanza masomo.

Dkt.Mganga amesema kuwa Mwaka huu peke yake zaidi ya wanafunzi elfu 90 wanatarajiwa kuanza masomo ambapo Mpaka kufikia Januari 26.2023 asilimia 89.7 ya wanafunzi wa darasa la awali walioripoti shule,huku asilimia 94.2 Kwa darasa la kwanza na asilimia 66.95 kidato Cha kwanza wakiwa wameripoti shule.

Naye Mratibu wa Program ya SHULE BORA Mkoa wa Dodoma Mtemi Zombwe amesema kuwa ili kufanikisha mchakato wa kuinua na kuboresha elimu ni vyema kila mmoja akatambua kuwa anajukumu la kushiriki katika mchakato huo.

"Mradi wa SHULE BORA ni Programu mahususi kabisa kwa ajili ya kuinua na kuboresha ubora wa elimu hivyo ili tufaniliwe ni lazima kila mmoja ajue ana wajibu wa kuhakikisha elimu inakuwa bora,"

Na kuongeza kuwa "Wazazi au jamii kwa ujumla ni lazima washirikiane na Serikali ama walimu katika masuala mbalimbali ikiwemo kuhakikisha miundombinu inaborshwa kwa upande wa kujifunzia,kufundishia alafu pia iwe Jumuishi pamoja na kuhakikisha mifumo ya elimu inaimarishwa kwa hapo tutakuwa tunaboresha na kuinua elimu yetu kila mmoja ashiriki,"Amema Zombwe

Zombwe ametoa wito kwa waandishi wa habari kufanya kazi ya kuhamasisha,kuelimisha na kuhabarisha jamii juu ya Mradi wa SHULE BORA na kwa namna gani inachochea ubora wa elimu hapa nchini.

Mratibu huyo amebainisha kuwa katika ngazi ya kitaifa SHULE BORA itatoa pia msaada wa kiufundi kwa serikali ya Tanzania, pamoja na utekelezaji wa mradi wa pili wa LIPWA KWA MATOKEO yaani Education Program for Results Two.

"Mradi unalenga kuwa na matokeo makubwa na endelevu katika elimu ,kwa kusaidia kuanzisha na kuimarisha mifumo na taratibu za elimu ,kwa kufanya hivyo ,mpango utaimarisha matokeo ya ujifunzaji,hususani katika KKK na kiwango cha wanafunzi kusailia shule,"amesema Zombwe
Mradi wa SHULE BORA utatekelezwa katika mikoa 9 ikiwemo Dodoma,Mara,Katavi,Rukwa,Kigoma,Singida,Simiyu,Pwani na Tanga hadi ifikapo mwaka 2027 kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid kwa gharama ya poundi za Kiingereza milion 89 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 271.


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa