• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RAS Dodoma awataka watumishi Kondoa Mji kufanya kazi kwa umahiri

Tarehe iliyowekwa: March 26th, 2024

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndg. Kaspar Mmuya amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Kondoa kufanya kazi kwa umahiri kwenye utendaji wao wa kazi kwa kuwa wote wamesoma wana sifa ndio maana wameajiriwa.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao na Wakuu wa Divisheni, vitengo, Watendaji wa Kata na Mitaa na watumishi wa makao makuu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji hivi karibuni.

“Umahiri siku zote unajengwa kwa kufanya, umahiri unajengwa siku zote kwa kuelewa jambo na kuboresha katika utendaji wako unapofanya vile ndio unajenga umahiri wako na hutofautiana mtu na mtu na ndio maana watu wanasema huyu anafanya vizuri sababu ujuzi wake anafanya kwa vitendo hatimaye anakuwa mahiri kwenye hilo eneo,”amesema RAS Mmuya

Amesema mtumishi asiyetaka kujishughulisha atakuwa afisa jina na hatakuwa anajua lolote kwa kuwa anamtegemea mtu na kusingizia kila kitu anajua Mkurugenzi kwa kuwa yeye si msemaji wa taasisi hivyo aulizwe Mkurugenzi hivyo yeye kama Katibu Tawala atanyooka na mtumishi huyo kwa kuwa ana ruhusa ya kumpigia mtumishi yoyote na kuomba taarifa yoyote na mtumishi anapaswa kutoa taarifa ya ukweli juu ya eneo analolisimamia.

“Usishtuke kwanini Katibu Tawala amenipigia simu hapana nakupigia kwasababu wewe ni mtumishi mwenzangu mwenye dhamana ya kufanya jambo fulani nakupigia kwa kuwa nahitaji taarifa ya haraka ili unitumie niitumie kukuwakilisha kutoa taarifa ya ubora ulioufanya katika eneo lako, sasa ukiniambia sijui mi nitakushangaa ila sintasema sijui na nitakutetea sababu moja ya jukumu langu ni kukutetea na kukulinda wewe sababu nilipokuja nilikabidhiwa watumishi,”amesema RAS Mmuya

Aidha amewataka Wakuu wa divisheni na vitengo kuhakikisha wanajulikana na kuitangaza Halmashauri kwa kukusanya mapato kupitia kodi mbalimbali na kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato kwa kuhakikisha wanamshauri Mkurugenzi kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kukusanya mapato mengi.

Ameongeza kwa kuwataka kusimamia fedha za miradi zinazoletwa katika Halmashauri kwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na kuweka mipango na kutenga fedha za kununua madawati na kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini na kuweka mipango pamoja na wazazi ya kumaliza utoro wanafunzi kuanzia elimu msingi hadi sekondari.

“Kukaa pamoja kuna faida zake ukiwa unakaa kwenye kazi usiwe na misimamo mnoo fanya kazi zako lakini kenye mahusiano kutakusaidia kazi zako zitekelezwe vizuri, ukitaka kufanikiwa fanya kazi kwa asilimia 20 na chukua asilimia 80 kwenye mahusiano sababu katika maisha tunategemeana na siwezi kufahamu mapungufu yangu na madhaifu yangu kama siwezi  kuinteract na mtu,”amesisitiza RAS Mmuya

Akiongea kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ndg. Said Majaliwa amemshukuru Katibu Tawala kwa kufika katika Halmashauri ya Mji Kondoa na kuwa Halmashauri ya pili kuitembelea toka kuteuliwa kwake na kumuahidi kuyafanyia kazi yote ambayo ameyatolea maelekezo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.

Katika ziara yake Katibu Tawala ameongoaza na wataalam mbalimbali kutoka ofisi yake ambapo pia amefanya ukaguzi wa miradi ya nyumba ya Mkurugenzi ulio katika hatua za ukamilishaji wenye thamani ya shilingi milioni 150 na Hospitali ya Mji Kondoa ambao umekamilika na una thamani ya shilingi milioni 900.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa